Nenda kwa yaliyomo

Shelisheli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamuhuri ya Ushelisheli
République des Seychelles (Kifaransa)
Repiblik Sesel (Kimaori)
Kauli Mbiu
"Finis Coronat Opus" (Kilatini)
"Mwisho hutunuku taji kazi"
Wimbo wa taifa
"Koste Seselwa"
Join together all Seychellois
Ramani ya
Ramani ya

Eneo la Seychelles

Mji Mkuu Victoria (Shelisheli)
Jiji kubwa Victoria (Shelisheli)
Kabila
  • 97% Wakrioli wa Shelisheli
  • 3.0% Wengine
Aina ya Serikali Jamhuri ya rais wa Umoja
Rais
Wavel Ramkalawan
Makamu wa Rais Ahmed Afif
Idadi ya Watu
Mwaka wa Makisio
Idadi ya watu (makisio) 130,523
Pato la Taifa PPP
Mwaka wa Makisio 2023
Jumla increase $4.175 bilioni USD (ya ya 177)
Capita increase $41,828
Pato la Taifa
Mwaka wa Makisio 2024
Jumla increase $2.085 bilion (ya ya 50)
Capita increase $20,889
Kiashiria cha Maendeleo ya Watu (2022) 0.802 (ya 67)
Maendeleo ya Juu Sana
Eneo la saa UTC+04:00 (SCT)
Nambari ya mwito +248


Shelisheli, kwa jina rasmi Jamhuri ya Ushelisheli (Kifaransa: République des Seychelles; Krioli Repiblik Sesel), ni nchi ya visiwa na taifa la visiwa linalojumuisha visiwa 155 (kulingana na Katiba) katika Bahari ya Hindi. Mji mkuu wake na mji mkubwa zaidi, Victoria (Shelisheli), uko kilomita 1,500 (milia za baharini 800) mashariki ya bara la Afrika. Nchi za visiwa na maeneo ya jirani ni Komoro, Madagaska, Morisi, na idara za ng'ambo za Ufaransa za Mayotte na Réunion kusini; na Archipelago la Chagos upande wa mashariki. Seychelles ni nchi iliyo ndogo zaidi barani Afrika pamoja na nchi ya Kiafrika iliyo na idadi ndogo zaidi ya watu, ikiwa na idadi ya watu inayokadiriwa kuwa 100,600 mwaka 2022

Ramani ya Shelisheli
Mji mkuu Victoria

Shelisheli ni funguvisiwa na jamhuri katika Bahari Hindi, mashariki kwa mwambao wa Afrika Mashariki na kaskazini kwa Madagaska.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Visiwa vya Shelisheli kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Shelisheli ina visiwa 115; 32 kati ya hivyo ni visiwa vikubwa kidogo vyenye milima, vingine ni vidogo na huitwa "Visiwa vya nje".

Kisiwa kikubwa zaidi ni Mahé na mji mkuu Victoria uko huko. Wakazi wengi huishi Mahe pamoja na visiwa vya karibu, hasa Praslin na La Digue.

Visiwa hivyo vina milima inayofikia hadi mita 900 juu ya UB. Mkubwa ni Morne Seychellois wenye mita 905 juu ya UB.

Hali ya hewa ni ya kitropiki ikiwa halijoto iko kati ya 24 °C na 30 °C. Kiasi cha mvua ni kati ya mm 2.880 huko Victoria na mm 3.550  mlimani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hakuna hakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu.

Taarifa ya kwanza imepatikana kutoka kwa Wareno waliozunguka hapa kuanzia mwaka 1505.

Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa au kukusanya matunda bila ya kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.

Ndio Ufaransa uliojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wao wa siku zile Jean Moreau de Sechelles.

Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe.

Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Waingereza walivumilia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.

Kwanza Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius, lakini mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni mbali na Mauritius.

Mwaka 1970 Shelisheli walipata uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uingerezeza lakini mwaka 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja.

Tangu 1993 katiba ilisahihishwa tena ikiruhusu vyama vingi vya kisiasa.

Chama kilichopata kura nyingi ndicho SPPF (Seychelles People's Progressive Front).

Wakazi kwa jumla (93.2%) ni machotara wenye mchanganyiko wa damu ya Afrika bara, Ulaya na Asia. Licha ya hao kuna vikundi vidogo vya Wahindi (6%), Wazungu (5%) na Wachina (0.5%) halisi.

Lugha rasmi ni tatu: Kiingereza (5.1%), Kifaransa (0.7%) na Kiseselwa, aina ya Krioli ambayo imetokana na Kifaransa na ndiyo lugha ya kawaida (91%).

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (76.2%), halafu Waprotestanti (13.0%), wengine wachache ni Wahindu (2.4%), Waislamu (1.6%) n.k.

Biashara ya Shelisheli inategemea hasa utalii unaoingiza 70% ya pato la taifa. Asilimia 30 hivi za wafanyakazi wote wamo katika utalii.

Pamoja na utalii, uvuvi na kilimo ni muhimu pia.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Dini
Taarifa za jumla

Shelisheli travel guide kutoka Wikisafiri

Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Shelisheli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.