Elizabeth II wa Uingereza

(Elekezwa kutoka Elizabeth II)
Kuhusu malkia mwingine mwenye jina hili ona Elizabeth I wa Uingereza

Elizabeth II alikuwa malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania (Uingereza na Welisi na Uskoti) na Ireland Kaskazini tangu mwaka 1952 hadi kufariki dunia tarehe 8 Septemba 2022. Alikuwa malkia kwa miaka 70 na siku 214. Katika historia yote ya dunia wako watawala wachache waliodumu madarakani muda mrefu kuliko yeye[1][2]. Soma zaidi wasifu wake hapa Anafuatwa na mwana wake wa kwanza, Charles III wa Uingereza.

Elizabeth Alexandra Mary
malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania (Uingereza, Welisi, Uskoti) pamoja na Ireland Kaskazini
malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania (Uingereza, Welisi, Uskoti) pamoja na Ireland Kaskazini
Tarehe ya kuzaliwa 21 Aprili 1926
Mahali pa kuzaliwa Mayfair, Uingereza
Ufalme wa Muungano
Tarehe ya kifo 8 Septemba 2022 (umri 96)


Elizabeth II mwaka 2006.

Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.

Alitangazwa kuwa malkia tarehe 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha baba yake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni la Uingereza akatembelea milima ya Aberdare.

Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.

Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola alikuwa pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo ndani ya jumuiya hii[3]:

Katika nchi zote aliposhika cheo hakuwa na mamlaka ya kiserikali ila alitawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.

Marejeo

  1. Queen Elizabeth II dies aged 96 Guardian (UK), 08.09.2022
  2. Mfalme Louis XIV wa Ufaransa alitawala miaka 72 kutoka 1643 - 1715; orodha hii inaonyesha wengine
  3. mbali ya nyingine ambazo katikati waligeuka Jamhuri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth II wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.