Thabo Mbeki
Thabo Mbeki | |
Rais wa Afrika Kusini (1999–2008)
| |
Deputy | Jacob Zuma Phumzile Mlambo-Ngcuka |
---|---|
mtangulizi | Nelson Mandela |
aliyemfuata | Kgalema Motlanthe |
Makamu wa Rais wa Afrika Kusini (1994–1999)
| |
Rais | Nelson Mandela |
aliyemfuata | Jacob Zuma |
tarehe ya kuzaliwa | 18 Juni 1942 Mbewuleni, Afrika Kusini |
chama | African National Congress |
ndoa | Zanele Dlamini Mbeki |
watoto | Monwabise Kwanda |
mhitimu wa | University of London University of Sussex |
Thabo Mvuyelwa Mbeki (amezaliwa 18 Juni 1942) alikuwa Rais wa nchi ya Afrika Kusini tangu 14 Juni 1999 hadi 24 Septemba 2008. Alimfuata Nelson Mandela.
Mbeki alilelewa katika familia ya Waxhosa katika jimbo la Rasi Mashariki. Wazazi walikuwa walimu wa shule na wanachama wa ANC.
Mwanaharakati wa ANC
[hariri | hariri chanzo]Thabo alishiriki katika shughuli za chama hiki wakati alipokuwa mwanafunzi. Baada ya kukamatwa kwa Nelson Mandelea na viongozi wengine wa ANC alitoka nchini akapelekwa Uingereza aliposoma elimu ya uchumi kwenye chuo kikuu cha Sussex. Baada ya masomo akajiunga na utumishi wa ANC na tangu 1971 alichaguliwa katika kamati kuu akawa mwakilishi wa ANC katika nchi mbalimbali za Afrika.
Tangu 1989 Mbeki alikuwa katibu wa chama mambo ya nje akahudhuria katika majadilioano kati ya serikali ya Afrika Kusini na ANC kuhusu namna za kumaliza sera ya Apartheid.
Makamu wa Rais na Rais
[hariri | hariri chanzo]Baada ya uchaguzi huru wa kwanza nchini Afrika Kusini mwaka 1994 alikuwa makamu wa rais chini ya Nelson Mandela. Mwaka 1997 akawa mwenyekiti wa ANC badala ya Mandela. 16 Juni 1999 akaapishwa kama rais wa Afrika Kusini akarudishwa katika uchagizi wa Aprili 2004.
Katika Desemba 2007 Mbeki aligombea tena nafasi ya mwenyekiti wa ANC lakini alishindwa na Jacob Zuma. Zuma pia alimfuata Mbeki kama Rais wa Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa 2009.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thabo Mbeki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |