Nenda kwa yaliyomo

Bob Marley

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bob Marley
Black and white image of Bob Marley on stage with a guitar
Marley akitumbuiza mnamo mwaka wa 1980
AmezaliwaRobert Nesta Marley
(1945-02-06)6 Februari 1945
Amekufa11 Mei 1981 (umri 36)
Miami, Florida, Marekani
Sababu ya kifoMetastatic melanoma
Majina mengine
  • Donald Marley
  • Tuff Gong
Asili yakeTrenchtown, Kingston, Jamaica
Kazi yake
  • Mwimbaji
  • mtunzi wa nyimbo
  • mwanamuziki
  • mpiga gitaa
DiniRomani Katoliki (1945–66)
Rastafari (1966–80)
Ethiopian Orthodox (1980–81) Kabatizwa kama MRastafari
NdoaAlpharita Anderson Marley (m. 1966–1981) «start: (1966-02-10)–end+1: (1982)»"Marriage: Alpharita Anderson Marley to Bob Marley" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Bob_Marley)
WatotoSharon Marley Prendergast (wakuasili)
Cedella Marley
David Nesta "Ziggy" Marley
Stephen Robert Nesta Marley
Rohan Anthony Marley
Julian Ricardo Marley
Ky-Mani Marley
Damian Robert Nesta Marley
WazaziNorval Sinclair Marley
Cedella Malcolm Booker
Musical career
Ala
  • Sauti
  • gitaa
  • tumba
Miaka ya kazi1962–1981
Studio
Ameshirikiana naBob Marley and the Wailers
Wavutibobmarley.com

Robert Nesta "Bob" Marley (6 Februari 1945 - 11 Mei 1981) alikuwa mwimbaji na mwanamuziki muhimu kutoka nchini Jamaika. Alivuma hasa kunako miaka ya 1970 na 1980. Ameweza kuifanya staili ya muziki wa reggae kuwa maarufu sana duniani. Muziki wake mwingi ulikuwa unazungumzia hadithi za nyumbani kwake na dini ya Rastafari ambayo yeye alikuwa anaifuata. Kuna baadhi ya nyimbo zake zinahusu masuala ya dini na zingine siasa.

Bob Marley alizaliwa na mama mweusi kijana aliyeitwa Cedella Booker na baba wa Kizungu aliyeitwa Norvall Marley. Wakati yungali bwana mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani kama "Tuff Gong".[1] Alianza kazi zake za muziki kunako miaka ya 1960 hivi akiwa na kundi lake la kina [[Wailing Wailers]], ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza zilizoitwa "Judge Not" na "One Cup of Coffee".

Bob alimwoa Bi. Rita Anderson mnamo 1966 na akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji. Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu sana.

Mwaka wa 1974, kundi la Wailers likavunjika kwa sababu wanachama wote watatu walitaka kujiendeleza kila mtu awe msanii wa kujitegemea. Lakini, Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya na kuindelea kupiga muziki kama kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa kibao chake cha kwanza kilichovuma kimataifa na kiliitwa "No Woman No Cry". Huko Jamaika, huhesabiwa kama kama shujaa wa jadi.

Baadhi ya vibao vyake vikali ni pamoja na "I Shot the Sheriff", "No Woman, No Cry", "Could You Be Loved", "Stir It Up", "Jamming", "Redemption Song", "One Love" na, "Three Little Birds",[2]. Albamu za studio ambazo ni maarufu kuliko ni ile iliyoitwa Legend, ambayo pia ina jumlisha vibao vyake vikali. Bob Marley alikufa tar. 11 ya mwezi wa Mei 1981, katika hospitali ya Cedars of Lebanon Hospital huko mjini Miami, Florida, kwa tatizo la melanoma (kansa ya ngozi).


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bob Marley kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.