Bolivia
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kihispania: ¡Morir antes que esclavos vivir! ("Heri kufa kuliko kuishi kama watumwa") | |||||
Wimbo wa taifa: Bolivianos, el hado propicio | |||||
Mji mkuu | Sucre | ||||
Mji mkubwa nchini | Santa Cruz | ||||
Lugha rasmi | Kihispania, Kiguarani, Kiquechua, Kiaymara | ||||
Serikali | Jamhuri Luis Arce | ||||
Uhuru Kutoka Hispania |
6 Agosti 1825 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,098,581 km² (ya 28) 1.29% | ||||
Idadi ya watu - 25 Machi 2014 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
10,556,102 (ya 83) 8,280,184 9/km² (ya 221) | ||||
Fedha | Boliviano (BOB )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
— (UTC-4) — (UTC?) | ||||
Intaneti TLD | .bo | ||||
Kodi ya simu | +591
- |
Bolivia (jina linatokana na shujaa Simon Bolivar) ni nchi isiyo na mwambao wa bahari katika Amerika Kusini.
Imepakana na Brazil, Paraguay, Argentina, Chile na Peru.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Nchi inakatwa na safu mbili za milima ya Andes zenye kimo hadi mita 6500 juu ya UB.
Nyanda za juu (kwa Kihispania: "Altiplano") zinakaliwa na wakazi wengi (80%) ziko kwenye kimo cha mita 3.000 hadi 4.000. Altiplano ni takriban theluthi moja ya eneo la nchi; sehemu nyingi ni tambarare ya "llanos" ambayo ni nchi ya chini yenye joto ambayo ina sehemu mbili: savana kavu za Gran Chaco na misitu minene ya beseni ya Amazonas.
Ziwa la Titicaca liko kwenye Altiplano.
Bolivia ni kati ya nchi maskini zaidi za Amerika Kusini.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Tofauti na nchi nyingine za bara hilo, wakazi asilia (Waindio) ni sehemu kubwa ya wananchi (55%), wakifuatwa na machotara (30%) na watu wenye asili ya Ulaya (15%).
Lugha rasmi ziko 37, kuanzia Kihispania na lugha nyingi asilia.
Upande wa dini, Kanisa Katoliki linaongoza (78%), likifuatwa na Uprotestanti (19%).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kihispania) Serikali ya Bolivia tovuti rasmi Ilihifadhiwa 11 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Bolivia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bolivia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |