Nenda kwa yaliyomo

Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ni siku ya kimataifa ambayo huadhimishwa kila tarehe 3 Disemba ya kila mwaka. Mwanzoni ilikuwa ikijulikana kama siku ya kimataifa ya Walemavu lakini kufikia mwaka 2007 siku hii ilibadilishwa jina.[1]

Siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 1992 na Umoja wa Mataifa, na tangu kuanzishwa kwa siku hii kumekuwa na mafanikio mbalimbali duniani.

Malengo ya siku hii ni kuongeza uelewa juu ya mambo yanayohusu watu wenye Ulemavu pamoja na kutoa elimu juu ya haki zao pamoja na hali njema, lakini pia, siku hii hutazamiwa kuongeza uelewa kwa watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali kama vile Uraia, siasa, uchumi na utamaduni. Kila mwaka siku hii huja na malengo tofauti tofauti.

  1. "International Day of Persons with Disabilities". Iliwekwa mnamo 4 Desemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)