Lagos
Lagos ni mji mkubwa wa Nigeria. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi mwaka 1991.
Ikiwa na wakazi takriban milioni 12 katika eneo la jiji na milioni 15 - 22 katika rundiko la mji ni kati ya miji mikubwa zaidi ya Afrika; inawezekana kwamba idadi ya watu imeshapita ya Kairo, hivyo kuwa jiji lenye watu wengi barani Afrika[1].
Lagos ilianzishwa kama mji wa bandari uliokua juu ya visiwa vidogo karibu na mdomo wa wangwa wa Lagos unapounganika na Bahari ya Atlantiki.
Bandari ya Lagos iko kati ya bandari muhimu zaidi Afrika[2][3].
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Lagos iko mwambaoni mwa Ghuba ya Guinea; wenyeji hutofautiana sehemu mbili kuu ambazo ni "kisiwani" (The Island) na "barani" (Mainland).
Lagos kisiwani
[hariri | hariri chanzo]Lagos kisiwani ni zaidi ya kisiwa kimoja, jina hili linajumlisha pande zote zilizotengwa na bara kwa mfereji ambao ni mlango wa wangwa wa Lagos kwenda baharini.
Visiwa vikubwa ni Lagos Island, Ikoyi, na Viktoria pamoja na visiwa vidogo mbalimbali, mara nyingi mifereji midogo kati yake imeshafunikwa kwa majengo na madaraja mengi au kujazwa. Sehemu hii ni kitovu cha biashara na maofisi pamoja na makazi yenye bei za juu.
Madaraja matatu makubwa huunganisha sehemu ya kisiwani na bara ambazo ni madaraja ya Carter, Eko na daraja la tatu la bara.
Lagos bara
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wengi wa Lagos huishi barani, ng'ambo ya wangwa. Huko viko viwanda vingi.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Hadi mwaka 2006 kulikuwa na manisipaa ya Lagos iliyojumlisha Lagos Visiwani pamoja na maeneo machache barani. Mwaka ule manisipaa ilivunjika na kugawiwa kwa halmashauri mbalimbali. Hali halisi jiji likaendelea kukua barani. Tangu siku zile serikali inalenga kuimarisha utawala kwenye ngazi za chini.
Ndani ya eneo la Lagos hakuna muundo wa manisipaa au jiji moja bali kuna halmashauri 16 zinazoitwa Local Government Area (LGA) na kuunganishwa katika "Metropolitan Lagos". Idadi za wakazi hapa chini zinarejea sensa ya 21 Machi 2006.[4]
Halmashauri ("LGA") | Eneo in km² |
Idadi ya wakazi (2006) |
Wakazi kwa km² |
---|---|---|---|
Agege | 11,20 | 459.939 | 41.066 |
Ajeromi-Ifelodun | 12,33 | 684.105 | 55.483 |
Alimosho | 185,20 | 1.277.714 | 6.899 |
Amuwo Odofin | 134,58 | 318.166 | 2.364 |
Apapa | 26,66 | 217.362 | 8.153 |
Eti-Osa | 192,35 | 287.785 | 1.496 |
Ifako-Ijaye | 26,61 | 427.878 | 16.080 |
Ikeja | 46,16 | 313.196 | 6.785 |
Kosofe | 81,41 | 665.393 | 8.173 |
Lagos Island | 8,66 | 209.437 | 24.184 |
Lagos Mainland | 19,47 | 317.720 | 16.318 |
Mushin | 17,48 | 633.009 | 36.213 |
Ojo | 158,16 | 598.071 | 3.781 |
Oshodi-Isolo | 44,76 | 621.509 | 13.885 |
Shomolu | 11,55 | 402.673 | 34.863 |
Surulere | 23,00 | 503.975 | 21.912 |
Gesamt | 999,58 | 7.937.932 | 7.941 |
Tabianchi
[hariri | hariri chanzo]Lagos huwa na tabianchi ya savana tropiki (Aw) kufuatana na upambanuzi wa Koeppen. Kiwango cha mvua kinatofautiana sana baina ya majira ya mvua na ya ukame. Masika (yenye mvua) yaanza mwezi Aprili na kuishia Oktoba. Ya ukame yako kati ya Novemba hadi Machi. Mwezi wenye mvua nyingi ni Juni yenye usimbishaji wa mm 315.5, ilhali Januari ina milimita 13.2 pekee.
Lagos iko karibu na ikweta, tena kwenye uwiano wa bahari, hivyo hakuna tofauti kubwa katika halijoto kati ya miezi ya mwaka. Wakati wa Machi wastani uko kwenye sentigredi 28.5 na Agosti huwa na 25.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kiasili eneo la Lagos lilikaliwa na kabila la Waawori ambao ni sehemu ya Wayoruba. Katika karne ya 15 ikaitwa "Oko".[5][6]
Chini ya chifu wao Olofin hao Waawori wakahamia kwenye visiwa ndani ya wangwa pamoja na Kisiwa cha Lagos[7]Francesca Locatelli - Paul Nugent, African Cities: Competing Claims on Urban Spaces, 2009, Brill, ISBN 978-9-0041-6264-8, page 114</ref>
Katika karne ya 16 eneo lilitwaliwa na milki ya Benin na kisiwa cha Lagos kilikuwa kambi la kijeshi la Benin kilichoitwa "Eko".[8][9] Jina hili linatumiwa hadi leo na wenyeji wa Lagos.
Jina la Lagos lilitumiwa na mabaharia Wareno waliojenga huko kituo cha biashara na kukiita kwa heshima ya mji wa Lagos huko Ureno[10].
Mwaka 1472 baharia Mreno Ruy de Sequeira alifika Eko akaanzisha kituo cha "Lagos" - kwa Kireno neno hili lamaanisha "maziwa": ni pia jina la mji wa Ureno ya kusini.
Katika karne zilizofuata Lagos ilikuwa ufalme mdogo wa Kiyoruba. Mtawala wake alistawi na kutajiriki kutokana na biashara na wafanyabiashara kutoka Ulaya. Sehemu kubwa ilikuwa biashara ya watumwa.
Katika karne ya 19 Uingereza ilibadilisha msimamo wake kuhusu utumwa wakijaribu kukandamiza biashara hiyo katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1841 Oba mpya aliyeitwa Akitoye alipiga marufuku biashara ya watumwa lakini alipinduliwa kwa sababu ya upinzani wa wafanyabiashara wenyeji. Akitoye aliomba usaidizi wa Uingereza. Manowari za Kiingereza zilishambulia Lagos tarehe 26 na 27 Desemba 1852 na kumrudisha mfalme.
Matatizo ya biashara ya watumwa yaliendelea na Waingereza walichukua kisiwa cha Lagos na kuifanya kwanza eneo lindwa halafu koloni. Oba alibaki na madaraka machache.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Lagos ni kitovu cha uchumi wa Nigeria. Kiasi kikubwa cha pato la taifa kinazalishwa hapa. Makao makuu ya makampuni makubwa na benki yako Lagos Kisiwani.
Lagos ni pia moyo wa tasnia ya mawasiliano (ICT) ya Afrika ya Magharibi. [11]
Sehemu za Lagos zina hali ya juu[12][13], hata hivyo theluthi mbili za wakazi huishi katika mitaa ya vibanda pasipo maji ya bomba na vyoo vya kutosha. [14]
Bandari ya Lagos ni bandari kubwa ya Nigeria iko pia kati ya mabandari makubwa ya Afrika. Ina pande tatu ambazo ni kando la kisiwa cha Lagos chenyewe halafu sehemu za Apapa (penye kituo cha kontena) na Tin Can.[15] Bandari imeunganishwa na mfumo wa reli ya Nigeria.
Sehemu muhimu ya biashara ya bandari ni petroliamu inayosafirishwa hapa kwenda kote duniani.[16] Mafuta ya petroli na bidhaa zilizotengenezwa kutoka mafuta hayo ni sawa na asilimia 14 za Jumla ya Pato la Taifa (GDP) na 90% za mapato ya fedha za kigeni.[17]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ linganisha worldpopulationreview.com inayorejea taarifa ya New York Times ya 2012; ilitazamiwa 23 Novemba 2016
- ↑ "Africa's biggest shipping ports", Businesstech. 8 March 2015. iliangaliwa 23 Novemba 2016
- ↑ "Africa's top 10 ports", arabianbusiness 12 Mei 2008, iliangaliwa 23 Novemba 2016
- ↑ GeoHive: Lagos - Administrative Units Archived 7 Agosti 2011 at the Wayback Machine..
- ↑ Margaret Peil (1991). Lagos: the city is the people (World cities series). G.K. Hall. uk. 5. ISBN 978-0-816-1729-93.
- ↑ Anthony Appiah; Henry Louis Gates (2010). Encyclopedia of Africa, Volume 1. Oxford University Press. uk. 28. ISBN 978-0-195-3377-09.
- ↑ Sandra T. Barnes (1986). Patrons and Power: Creating a Political Community in Metropolitan Lagos. Indiana University Press, International African Library. uk. 20. ISBN 978-0-2533-4297-3. Iliwekwa mnamo Julai 26, 2014.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Williams, Lizzie (2008). Nigeria: The Bradt Travel Guide. Bradt Travel Guides. uk. 110. ISBN 1-84162-239-7.
- ↑ Smith, Robert Sydney (1988). Kingdoms of the Yoruba (tol. la 3). University of Wisconsin Press. uk. 73. ISBN 0-299-11604-2.
- ↑ "The Origin of Eko (Lagos)". Edo Nation. Iliwekwa mnamo 2 Juni 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Douglas Zhihua Zeng (2008). Knowledge, Technology, and Cluster-based Growth in Africa (WBI development studies). World Bank Publications. uk. 66. ISBN 9780821373071.
- ↑ Tolu Ogunlesi. "Commercial hub status of Lagos sparks a chain reaction", Financial Times, May 4, 2014. Retrieved on March 17, 2016.
- ↑ "Luxury living in Lagos", CNBC Africa, October 21, 2013. Retrieved on March 16, 2016. Archived from the original on 2016-03-19.
- ↑ Lagos, the mega-city of slums
- ↑ "OT Africa Line – Nigeria Page". Otal.com. 1 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 2 Juni 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "OT Africa Line – Lagos Port Statistics" (PDF). Iliwekwa mnamo 2 Juni 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nigeria". CIA World Factbook. 1 Februari 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-31. Iliwekwa mnamo 4 Aprili 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lagos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |