Kisiwa cha Alexander
Kisiwa cha Alexander ni kisiwa kikubwa zaidi cha Antaktiki. Kiko kwenye Bahari ya Bellingshausen upande wa magharibi wa Rasi ya Antaktiki. Kimetengwa na rasi na mkono wa bahari unaoitwa "mfereji wa George VI" wenye upana wa km 24 hadi 64. [1]
Kisiwa cha Alexander kina urefu wa km 390; upana wake hubadilika kati ya km 80 kaskazini na km 150 kusini[2].
Eneo hili lilitembelewa na watu mara ya kwanza mnamo 28 Januari 1821 na wapelelezi kutoka Urusi. WaliIiita kwa heshima ya Tsar Alexander I wa Urusi. Wakati ule halikutambuliwa ni kisiwa, vali lilidhaniwa kuwa sehemu ya bara maana ngao ya barafu ya Antaktiki inandelea mfululizo kutoka bara kwa kufunika mkono wa bahari na kisiwa.
Mwaka 1940 lilitambuliwa ni kisiwa[3].
Kuna milima mirefu inayopanda hadi mita 2,987 juu ya usawa wa bahari. Sehemu ya pekee ni ziwa la maji matamu linalofunikwa na mita 4 za barafu muda wote, linaitwa Ziwa Hodgson. [4] [5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stewart, J. (2011) Antarctic An Encyclopedia McFarland & Company Inc, New York. 1776 pp.
- ↑ Alexander Island, tovuti ya Britannica, ilingaliwa Novemba 2019
- ↑ Antarctica Detail Ilihifadhiwa 8 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya U.S. Geological Survey, iliangaliwa Novemba 2019
- ↑ Hodgson D.A., S.J. Roberts, M.J. Bentley, J.A. Smith, J.S. Johnson, E. Verleyen, W. Vyverman, A.J. Hodson, M.J. Leng, A. Cziferszky, A.J. Fox, and D.C.W. Sanderson (2009) Exploring former subglacial Hodgson Lake, Antarctica Paper I. Quaternary Science Reviews. 28:23-24:2295–2309.
- ↑ Hodgson D.A., S.J. Roberts, M.J. Bentley, E.L. Carmichael, J.A. Smith, E. Verleyen, W. Vyverman, P. Geissler, M.J. Leng, and D.C.W. Sanderson (2009) Exploring former subglacial Hodgson Lake, Antarctica Paper II. Quaternary Science Reviews. 28:23-24:2310–2325.