Cherehani
Cherehani (pia: charahani; kutoka Kiajemi چرخ, charakh, "gurudumu" na خان, khan "nyumba"; kwa Kiingereza "sewing machine") ni mashine ya kushonea vitu kama kitambaa, nguo, viatu au mifuko.
Inatumia uzi kwa kuunganisha vipande viwili vya kitambaa au ngozi. Tofauti na ushonaji kwa mkono, cherehani hutumia nyuzi mbili, moja ya juu na nyingine ya chini, zinazounganishwa.
Cherehani ya kwanza ilitengenezwa wakati dunia ilipokuwa ikipata mfumo mpya wa kiufundi (industrial revolution). Ushonaji huu wa cherahani ulianznshwa ili kupunguza kazi za kushona zilizokuwa zikifanywa kwa mikono.
Cherehani ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1790 na mvumbuzi Mwingereza Thomas Saint na baadaye ikaendelea kuboreshwa ili iwe ya kufana Zaidi na kufanya kazi kwa haraka zaidi. Hadi hapo kushona kulifanywa kwa mkono kutengeneza suruali, mashati, viatu na nguo zilizo na sindano na nyuzi. Hivyo, historia ya mashine ya kushona haikuwepo bila sanaa ya zamani ya kushona kwa mkono ambayo imekuwapo zaidi ya miaka 10,000. Sindano ya kwanza ilifanywa na mifupa ya mifugo au pembe na nyuzi zilizotokana na mishipa ya wanyama.[1]
Siku hizi mwendo wa cherehani unatokana mara nyingi na injini ya umeme. Kuna pia vyerehani vinavyosukumwa kwa mguu au kwa mkono.
Siku hizi kuna aina nyingi kwenye viwanda zilizobuniwa kwa shughuli maalum. Baadhi ya mashine za kushona na zile za viwandani hutumia mnyororo.
Kuna cherehani aina mbili: zile za kushona nyumbani ambazo huwa ndogo na zingine zinazotumiwa katika makampuni ya kushonea nguo ambazo hufanya kazi kwa haraka na sanasana hutumia nguvu za stima.
Mashine ya kushona inaweza kufanya aina tofauti za kazi ambazo kwa mfano hujumuisha njia za kuburudisha, kushikilia na kusonga kitambaa chini ya sindano ya kushona ili kuunda muundo wa kushona.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Charles Fredrick Wiesenthal, mvumbuzi wa Ujerumani, aliumba "sindano iliyoundwa kwa mashine". Hakuna maelezo katika hati miliki yake ambayo inahusu mashine ya kushona, lakini haja ya uvumbuzi wake ni hivyo imeonyeshwa.
Hati miliki ya kwanza ya mashine ya kushona iliyotolewa kwa Thomas Saint iliundwa kushona ngozi na nguo, ilitumia nyuzi moja na kuunda kushona mlolongo miaka 35 kabla ya mhandisi Wiesenthal.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-06. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |