Wafiadini wa Lyon
Wafiadini wa Lyon ndio Wakristo wafiadini wa kwanza wa Ufaransa[1].
Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lugdunum (siku hizi Lyon).
Kati yao, ni maarufu hasa askofu Potinus wa Lyon na mtumwa bikira Blandina wa Lyon.
Wengine ni: Aleksanda, Attalus, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia.
Nusu yao walikuwa wenyeji, nusu nyingine walowezi kutoka Frigia, leo nchini Uturuki.
Wakiwa gerezani, walimuandikia Papa Eleuteri barua nzuri sana kuhusu kudumisha amani ya Kanisa[2].
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 2 Juni[3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kitabu V, I cha Historia ya Kanisa iliyoandikwa na Eusebi wa Kaisarea, kinapatikana katika site de l'antiquité latine et grecque
- Kitabu I, 49 cha Vitabu vitano vya miujiza kilichoandikwa na Gregori wa Tours, kinapatikana katika site de l'antiquité latine et grecque
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |