Nenda kwa yaliyomo

Aleksanda wa Lyon (+ 177)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aleksanda wa Lyon ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Lyon wanaoheshimiwa kama watakatifu.

Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lyon.

Kati yao, ni maarufu hasa askofu Potinus wa Lyon na bikira Blandina wa Lyon. Wengine ni huyo Aleksanda, halafu Attalus wa Lyon, Espagathus wa Lyon, Maturus wa Lyon, Sanctius wa Lyon na wengine 41. Baadhi walifia gerezani, baadhi waliuawa katika kiwanja cha michezo mbele ya maelfu ya watazamaji, ama kwa kwa kukatwa kichwa ama kwa kutupwa waliwe na wanyamapori.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 2 Juni[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.