Nenda kwa yaliyomo

Uyoga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kundi la muziki nchini Kenya tazama Uyoga (bendi)

Uyoga.

Uyoga ni sehemu ya kuvu inayotokea juu ya ardhi na kukuza vibufu vinavyofanana na mbegu ya mimea. Uyoga mara nyingi huitwa mimea lakini si mimea, ni sehemu ndogo ya kuvu (kwa Kilatini: fungi).

Kazi ya uyoga kwa fungi yake ni kama matunda kwa mmea yaani ni kusaidia kuzaa na kusambaza.

Uyoga ni sehemu ndogo tu ya fungi yote inayoendelea kama miseli ndani ya ardhi kwa mita nyingi.

Uyoga si fungi yenyewe bali kitu kama tunda lake. Unajengwa na nyuzi nyingi za kungunyanzi na kuwa mahali pa kukuza vibufu ambavyo ni kama mbegu ya fungi.

Uyoga kama chakula

[hariri | hariri chanzo]

Uyoga ni maarufu kama chakula, lakini ni chakula kinachohitaji uangalifu na utaalamu. Zinapikwa, kukaangwa na aina kadhaa pia huunganishwa bichi katika saladi.

Uyoga huwa na protini nyingi pamoja na madini na vitamini ndani yake. Kwa hiyo ni chakula bora.

Kwa upande mwingine kuna uyoga za sumu zinazofanana na uyoga za kuliwa, lakini sumu yake ni kali kiasi cha kuweza kuua.

Uyoga huvunwa pale zinapokua. Hizi zinauzwa barabarani au sokoni.

Aina kadhaa (kwa mfano champignon) zinalimwa kibiashara na kuuzwa kwenye maduka makubwa. Ni aina zinazofaa kutunzwa katika friji kwa siku kadhaa.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uyoga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.