Nenda kwa yaliyomo

Sikukuu za Bikira Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Bikira Maria wa Mateso huko Warfhuizen, Uholanzi.

Sikukuu za Bikira Maria ni siku za kalenda ya liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Kikristo zilizopangwa katika mwaka wa Kanisa[1] kufanya ukumbusho wa matukio ya maisha yake na mengineyo ya historia ya Kanisa.

Sikukuu hizo zinatofautiana kadiri ya imani ya madhehebu husika[2].

Heshima za Liturujia ya Kiroma kwa Maria

[hariri | hariri chanzo]

Katika liturujia ya Roma, mbali ya kumtaja Mama Bikira Maria katika kila Misa wakati wa sala ya ekaristi, kuna maadhimisho kwa heshima yake. Hapa yamepangwa kulingana na kiwango cha heshima hiyo:

Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya hiari ya Mama wa Mungu.

  1. Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria: mashariki zinatumika tenzi na nyimbo mbalimbali, k.mf. Akatistos inayomuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “ngazi aliyoiona Yakobo” “kina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Mwa 28:12); magharibi anaheshimiwa kwa rozari.
  2. Wakristo wanaomheshimu Bikira Maria wanajieleza kwamba hawamuabudu hata kidogo, lakini wanamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Tofauti ni kwamba Mungu tu anastahili kuabudiwa (kwa Kigiriki, ‘latria’) watakatifu wanapewa heshima (‘dulia’) na Bikira Maria heshima zaidi (‘yuper-dulia’). Kanisa Katoliki linakiri neema zote za Mungu zinampitia Maria.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]