Mlolongo wa Kitume
Mlolongo wa Kitume (kwa Kiebrania האפיפיור הירושה, kwa Kigiriki Αποστολική διαδοχή) ni jambo linalodaiwa na imani ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo, ya kwamba ni lazima viongozi wa Kanisa washiriki mamlaka ya Mitume wa Yesu katika mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono na maaskofu katika kuwapatia daraja takatifu.
Imani hiyo inatiwa maanani hasa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo.
Kwao, maaskofu wa leo ni waandamizi wa wale wa jana na juzi hata kurudia kwa wale waliowekewa mikono na mitume wenyewe katika karne ya 1.
Mlolongo huo unahakikisha uhalali wa mamlaka yao katika kufundisha, kutakasa na kuongoza.
Kwa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti, suala la mikono si la lazima, kwani kwao ni muhimu zaidi kuendeleza mafundisho ya mitume.
Vyanzo na viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Against Heresies, Online-text, Irenaeus, Against Heresies
- Apostolicity in the Catholic Encyclopedia
- Christian Cyclopedia article on apostolic succession
- Methodist Apostolicity Archived 4 Mei 2008 at the Wayback Machine. by Gregory S. Neal
- Methodist Episcopacy: In Search of Holy Orders (1990) Archived 15 Mei 2008 at the Wayback Machine. by Gregory S. Neal
- Scott Hahn on the Papacy Archived 9 Oktoba 2006 at the Wayback Machine. by Scott Hahn. Discusses "the chamberlain of the royal household of ancient Israel" or "Prime minister" of the "house of David" (Isaiah 22:22 Archived 9 Februari 2008 at the Wayback Machine.) vis-à-vis Dynastic Succession .
- Views on apostolic succession at WikiChristian
- "Was Wesley Ordained By Bishop Erasmus?" The Methodist Quarterly Review (1878) Archived 1 Desemba 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mlolongo wa Kitume kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |