Nenda kwa yaliyomo

Lucy Wilmot Smith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lucy Wilmost Smith

Lucy Wilmot Smith (Novemba 16, 1861 - Desemba 1, 1889) alikuwa mwalimu, mwanahabari, mwandishi wa majarida, na mwanahistoria wa Marekani. Alikuwa mmoja wa wanawake wachache kushika nafasi katika ofisi ya American National Baptist Convention ya Kisabato.[1] Arts and Feminism 2023

Elimu ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Lucy Wilmot Smith alizaliwa Novemba 16, 1861, huko Lexington, Kentucky, binti wa Margaret Smith. Ingawa haijulikani ikiwa alizaliwa kama mtumwa, nyumba yao ilikuwa ya kimaskini. Smith alisomeshwa na mama yake.

Mnamo mwaka 1877, akiwa bado kijana mdogo, alichukua nafasi chini ya Bodi ya Shule ya Lexington. Mnamo mwaka 1881, alichaguliwa kuwa mwalimu chuo cha Simmons College of Kentucky, akisimamia shule iyo kama mkuu. Kwa muda, aliwahi kuwa katibu wa faragha wa Dk. William J. Simmons, ambaye alisaidia kazi yake, akiongea mara nyingi juu ya umuhimu wa Smith na usaidizi wake. Ingawa alikuwa akihudumu kama mwalimu na katibu wa kibinafsi, alichukua masomo ya idara ya kawaida na akahitimu mnamo mwaka 1887. Alimsaidia kifedha dada katika chuo kikuu. Baada ya kuhitimu kwa dada huyu alichukua masomo, katika shule hiyo hiyo.

Mnamo mwaka 1884, Smith aliacha Chuo Kikuu cha Jimbo na kujaza nafasi ya kazi huko Wyandotte County, Kansas,Apa aliudumu kama mshonaji na kama msimamizi alirudi katika nafasi yake ya zamani katika Chuo Kikuu cha Jimbo, Septemba, 1885, ambapo alihudumu kama karani wa kifedha na mmishonari wa jiji. Alikuwa Mkristo, Desemba 1872, chini ya ushawishi wa Mchungaji James Monroe, na akajiunga na Kanisa la Baptist.

Wakati wito ulipotolewa mnamo mwaka 1883, na Simmons, kwa wanawake wa Baptist wa Jimbo kuja pamoja na kupanga kwa faida ya kazi ya elimu, Smith alikua katibu wa shirika. Alikuwa mwanachama wa Bodi ya Mameneja kwa miaka na alikuwa Katibu wa kituo cha kusaidia Vijana, msaidizi wa chombo hicho. Aliandika kijitabu cha kurasa 13, akielezea kazi, katiba, utaratibu wa biashara na vijana wanavyoweza kufanya ili kupata pesa zao. Mkutano wa kwanza National Baptist Convention, USA, Inc. | National Baptist Convention, ambao ulikutana huko St.Louis mnamo 1886, walisikiliza jarida kutoka kwake juu ya "The Future Colored Girl,," ambayo imechapishwa katika "Jarida "la mkutano huo. Alichaguliwa pia wakati huo kama Mwanahistoria wa chombo hicho, na aliitumikia miaka kadhaa kama mmoja wa Kamati ya Utendaji. Mnamo 1888, alionekana tena kwnye magazeti ambayo ilianza mnamo 1884, wakati alipodhibiti "safu ya watoto" katika "The American Baptist", ya Louisville. Mnamo mwaka 1887, alikubali kufanya kazi na "The Baptist Journal" ambayo Mchungaji R. H. Coles, wa St. Louis, alikuwa mhariri. Alitoa michoro ya waandishi wa magazeti, na "Mwandishi wa Habari wa New York", kwa maslahi ya wasanii, waandishi na wachapishaji, waliisifia Kazi yake.

Smith alivutiwa sana na kufanikiwa kwa wanawake na alikuwa akiongea sana juu ya mwanamke mwenye nguvu.Aliandika kitabu juu ya "Wanawake na Mafanikio yao," "Women and Their Achievements," na kiliungwa mkono.

Mnamo msimu wa mwaka 1888, kutokana na kufanya kazi kupita kiasi alianza kuugua kikohozi kilicho mfanya apumzike. Marafiki zake walimshauri ivyo. Zilifanywa jitihada nyingi na madaktari pamoja na marafiki zake kwani waliamini ikiwa atacha kazi itakua ni pigo kubwa sana kwao.Walakini aliendelea kufanya kazi. Majira ya kila joto yanapokuja, alienda likizo, lakini akiwa amechelewa sana kufanya mema mengi. Septemba, 1889, aliugua kazini na kuwa dhahifu sana jambo lililosababisha kifo chake. Dk Simmons ahubiri katika mazishi yake, na akachagua nyimbo na vifungu vya maandiko kwa hafla hiyo. Mama yake alitamani kuwa nae lakini haikuwezekana kwani alikata. Oktoba 15, 1889, alikubali kwenda nyumbani, na alikuwa ameongozana na Jane McKamey, na Mchungaji C. H. Parrish. Alikufa Desemba 1, 1889.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Gottlieb, Roger S. (2003). Liberating Faith: Religious Voices for Justice, Peace, and Ecological Wisdom. Rowman & Littlefield. ISBN 978-0-7425-2535-1.
  • Murphy, Larry G.; Melton, J. Gordon; Ward, Gary L. (20 Novemba 2013). Encyclopedia of African American Religions. Routledge. ISBN 978-1-135-51338-2.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Scruggs, Lawson Andrew (1893). Women of Distinction: Remarkable in Works and Invincible in Character (tol. la Public domain). L. A. Scruggs.
  1. Jones, Reinette (20 Februari 2017). "Notable Kentucky African Americans Database". University of Kentucky Libraries. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-21. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2017. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)