Nenda kwa yaliyomo

Ijumaa Kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msalaba wa Ijumaa Kuu kwenye Monasteri ya Utatu Mtakatifu, Meteora, Ugiriki.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki
Picha takatifu ya karne ya 16 ikionyesha tendo la kumsulubu Yesu kadiri ya Theophanes wa Krete (Stavronikita Monastery, Mlima Athos, Ugiriki).
Siku ya Ijumaa Kuu Wakatoliki wanapokea ekaristi ingawa Misa haiadhimishwi (Our Lady of Lourdes, Philadelphia, Marekani).
Njia ya Msalaba ikiadhimishwa kwenye Colosseum mjini Roma siku ya Ijumaa Kuu. Mwishoni, Papa anatoa neno.
Picha ya El Greco ikimuonyesha Yesu akibeba msalaba, 1580.
Epitafyo ya Kiorthodoksi ikionyesha mwili wa Yesu ukizikwa.
Epitafyo ikichukuliwa katika maandamano.

Ijumaa Kuu ni siku ya Ijumaa kabla ya Pasaka ambapo Wakristo wengi duniani wanaadhimisha kifo cha Yesu Kristo msalabani.

Kufuatana na taarifa za Injili nne katika Biblia ya Kikristo, Yesu alisulubiwa siku kabla ya Sabato (au Jumamosi), yaani Ijumaa. Mahali pa kumsulubisha palikuwa kilima cha Golgotha kilichokuwepo wakati ule nje ya kuta za mji wa Yerusalemu.

Kadiri ya Injili ya Mtume Yohane, kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kila mwaka. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wameweza kukadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.

Sikukuu hii haina tarehe thabiti katika kalenda ya kawaida. Ilhali hutangulia Pasaka inafuata pia mabadiliko ya tarehe za Pasaka. Pamoja na mapokeo yaliyo tofauti kati ya Ukristo wa Magharibi (Wakatoliki na Waprotestanti wengi) na Ukristo wa Mashariki (makanisa ya Kiorthodoksi na Wakatoliki wa Mashariki), kuna tarehe mbili tofauti za Pasaka, na hivyo pia kila mwaka kuna tarehe mbili tofauti za Ijumaa Kuu.

Mwaka Ukristo wa
Magharibi
Ukristo wa
Mashariki
2018 30 Machi 06 Aprili
2019 19 Aprili 26 Aprili
2020 10 Aprili 17 Aprili
2021 02 Aprili 30 Aprili
2022 15 Aprili 22 Aprili

Katika liturujia ya makanisa

[hariri | hariri chanzo]

Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.

Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake (Ijumaa), kulala kaburini (Jumamosi), na hatimaye kufufuka kwa utukufu (Jumapili), kwa ufupi:

  1. Yesu mteswa,
  2. mzikwa na
  3. mfufuka.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ijumaa Kuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.