Hori ya Baffin
Hori ya Baffin (kwa Kiingereza: Baffin Bay) ni mkono wa Bahari Atlantiki unaotenganisha Greenland na Kisiwa cha Baffin upande wa magharibi.
Jina la Baffin Bay linamaanisha "Hori ya Baffin" ingawa si hori, inafanana zaidi na mlangobahari mrefu sana.[1][2][3]. Ila tu, ilhali uso wake unafunikwa na barafu kwa sehemu ya mwaka, wapelelezi wa kwanza waliopeleka habari zake Ulaya waliuona kama hori.
Eneo la Hori ya Baffin ni mnamo Km² 689,000. Urefu wake kutoka kaskazini hadi kusini ni km 1,450 baina ya pwani ya Greenland na Kisiwa cha Baffin. Upana wake ni kati ya km 650 na km 110.
Sehemu yenye kina kirefu cha mita 2.100 inapatikana katikati.
Watu walikalia pwani za Baffin Bay kuanzia mwaka 500 BK. Wakazi wa kwanza hawajajulikana vizuri, walifuatwa na Waeskimo.
Waviking kutoka Norwei walifuata mnamo mwaka 1000 walipotea tena hadi mnamo mwaka 1300.
Waingereza walianza kutembelea eneo hilo mwaka 1585 walipotafuta njia ya kufika Asia kwa kupita Amerika upande wa kaskazini.
Bahari hii ilipokea jina kutokana na nahodha William Baffin aliyepeleleza sehemu kubwa mwaka 1612 na kuchora ramani za pwani zake hadi gredi 77° 45′ za kaskazini.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Baffin Bay Archived 13 Mei 2013 at the Wayback Machine., Great Soviet Encyclopedia (in Russian)
- ↑ Baffin Bay, Encyclopædia Britannica on-line
- ↑ Reddy, M. P. M. (2001). Descriptive Physical Oceanography. Taylor & Francis. uk. 8. ISBN 978-90-5410-706-4. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2010.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)