Historia ya Ufilipino
Historia ya Ufilipino inahusu historia ya visiwa ambavyo leo vinaunda jamhuri ya Ufilipino.
Wanegritos ni kati ya wakazi asilia ya funguvisiwa hilo, wakifuatwa na Waaustronesia.
Baadaye kukawa na athira ya Wachina, Wamalay, Wahindi na Wamori.
Mwaka 1543 nchi iliitwa na Ruy López de Villalobos kwa jina la Kihispania "Las Islas Filipinas" (Visiwa vya Filipo) kwa heshima ya mfalme Filipo II wa Hispania.
Hispania ilitawala eneo hilo tangu mwaka 1565 hadi Mapinduzi ya Ufilipino ya 1896, ikiacha athari kubwa upande wa dini na utamaduni.
Marekani ilitwaa visiwa hivyo mwaka 1898 katika Vita vya Marekani dhidi ya Hispania na kuvitawala kama koloni hadi Vita Vikuu vya Pili vya Dunia wakati Japani ilipotwaa nchi kwa miaka minne.
Baada ya vita hivyo Ufilipino ikapewa uhuru wake.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ufilipino kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |