Historia ya Kupro
Historia ya Kupro inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Kupro.
Kisiwa cha shaba
[hariri | hariri chanzo]Watu waliishi kisiwani huko walau kuanzia milenia ya 10 KK.
Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa.
Katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Kisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko.
Kuanzia mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji mizima.
Chini ya Waosmani
[hariri | hariri chanzo]Baada ya Wakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu, Waturuki Waosmani walikiteka mwaka 1570 na kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya wenyeji.
Chini ya Waingereza
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1878 Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914.
Uhuru
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 16 Agosti 1960 Kupro ilijipatia uhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana na Ugiriki au kugawiwa kati ya kaskazini (Waturuki) na kusini (Wagiriki).
Baada ya uhuru
[hariri | hariri chanzo]Tangu vita vya Kupro, 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa yanatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.
Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Kupro kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |