Yohane wa Triora
Mandhari
Yohane wa Triora (alizaliwa Francesco Maria Lantrua huko Molini di Triora, Italia, 15 Machi 1760) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti na padri aliyefia dini huko Changsha, Hunan, China tarehe 7 Februari 1816).
Kwanza aliteswa sana gerezani, halafu akanyongwa.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 1 Oktoba 2000, alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 27 Mei 1900.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |