Wilaya ya Kinondoni
Wilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam yenye postikodi namba 14000. Kwa lugha nyingine ni manispaa ndani ya jiji la Dar Es Salaam.
Eneo lake ni sehemu za kaskazini za jiji. Kinondoni inaanza upande wa pwani kwenye Selander Bridge juu ya mto Upanga (pia: Msimbazi Creek) na kuendelea kupitia rasi ya Msasani, Kunduchi hadi Mbweni pamoja na hoteli za kitalii zilizopo sehemu hizo.
Barani inaelekea kuvukia barabara ya Morogoro hadi Mbezi na Kibamba. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo ndani ya manispaa hii.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Kinondoni ilihesabiwa kuwa 1,775,049 [1]. Baada ya wilaya kumegwa, katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 982,328 [2].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sensa ya Tanzania ya 2012". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2010-10-30.
- ↑ https://www.nbs.go.tz
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Halmashauri ya Manisipaa ya Kinondoni (pamoja na ramani, takwimu n.k. Archived 4 Oktoba 2011 at the Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Kinondoni - Tanzania | ||
---|---|---|
Bunju • Hananasif • Kawe • Kigogo • Kijitonyama • Kinondoni • Kunduchi • Mabwepande • Magomeni • Makongo • Makumbusho • Mbezi Juu • Mbweni • Mikocheni • Msasani • Mwananyamala • Mzimuni • Ndugumbi • Tandale • Wazo |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kinondoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |