Nenda kwa yaliyomo

Vila Algarve

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vila Algarve

Vila Algarve ni nyumba ya makazi katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo . Jengo hilo lililojengwa mwaka 1934 na baadaye lililoorodheshwa katika majengo yanayotakiwa kuwekewa ulinzi kulindwa, lilindwa na polisi wa siri wa Ureno PIDE/DGS hadi mwisho wa kipindi cha ukoloni wa Ureno nchini Msumbiji . Iko kwenye makutano ya Avenida Mártires da Machava na Avenida Ahmed Sekou Touré .

Historia.

[hariri | hariri chanzo]

Jengo hili mwaka 1934 lilichaguliwa kuwa makazi ya Ureno. Kitu kilichokuwa kinashangaza ni vigae, kama mfano mdogo wa mapambo asilia ya vigae kuanzia mwanzo wa karne ya ishirini - pamoja na usanifu wa kihistoria[1].

Mwanzoni mwa vita vya makoloni ya Ureno ya Guinea, Angola na Msumbiji, Polisi wa siri wa Ureno (PIDE) walipanua shughuli zao kwenye maeneo ya makoloni. Polisi wa siri wa Ureno (PIDE) walinyang'anywa Jengo na kuweka makao hapo. Kipindi cha vita vya makoloni wapiganaji wapinzani wengi waliteswa ndani ya hili Jengo. Mtu mwenye asili ya Msumbiji Mshairi José Craveirinha aliongea uzoefu wake ndani ya hii nyumba kwenye kazi zake tatu[1][2]. Wengine wajulikanao kama wafungwa walikuwa Rui Knopfli na Malangatana Ngwenya kati ya wengine[3].

Baada ya Uhuru wa Msumbiji, Jengo lilibakia Tupu kutokana na historia yake; ikiwemo lisilo na makazi[4]. Mwaka 1999[5] muungano wa wanasheria wenye asili ya Msumbiji walilipata Jengo na kutazamia kuwa Makao makuu yawe hapo. Gharama ilikadiriwa kuwa 400,000 euros[3][6].Kwa Baadae, Muungano huo ulijiondoa kwenye matazamio yao na kushikiria kuwa Jengo la Wizara ya utamaduni. Badala ya kuwa Makazi ya Wizara, pakawa "Makumbusho ya ukombozi wa Msumbiji" eneo hilo[7][8].

Tangu mwaka 2011 Jengo hilo ni machaguo ya mwanzo kwa orodha ya makumbusho kwa Maputo. Kwenye Hifadhidata ya Mkumbusho ya Ureno Sistema de Informação para Património Arquitectónico, ambapo pia ilihusisha kazi za waliokuwa makoloni ya Ureno, lilikuwa limesajiliwa kwa namba 31730[1].

Marejeo.

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 "Monumentos". www.monumentos.gov.pt (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  2. Não sei se é uma medalha (1967), Vila Algarve (1ª versão) (1988) and Vila Algarve (2ª versão) (1998)
  3. 3.0 3.1 "Ordem dos Advogados reabilita antiga sede da PIDE em Maputo - dn - DN". web.archive.org. 2015-04-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-02. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-27. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  5. "Moçambique: Ordem dos Advogados quer transformar edifício da PIDE em ″sede dos direitos e dignidade humanas″". www.jn.pt (kwa Kireno (Ulaya)). Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  6. "Ordem dos Advogados vai assumir "Vila Algarve" - garante o novo Bastonário, Gilberto Correia". Moçambique para todos. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  7. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-09. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  8. "Vila Algarve será museu da Luta de Libertação". Moçambique para todos. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.