Nenda kwa yaliyomo

Thugz Mansion

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Thugz Mansion”
“Thugz Mansion” cover
Single ya 2Pac akishirikiana na Nas na J. Phoenix
kutoka katika albamu ya Better Dayz na God's Son
Imetolewa 17 Januari 2002
Muundo CD
Imerekodiwa 2001
Aina Hip hop
Urefu 4:12
Studio Amaru
Mtunzi Tupac Shakur
Mtayarishaji 7 Aurelius na Kon Artis (7" Remix version)
A. Pittboss Johnson, Aulsondro "Novelist" Hamilton, Claudio Cueni and Michael Herring (Acoustic Version)
Mwenendo wa single za 2Pac akishirikiana na Nas na J. Phoenix
"Letter 2 My Unborn"
(2002)
"Thugz Mansion"
(2002)
"Still Ballin"
(2002)

"Thugz Mansion" ni wimbo ulioimbwa na msanii wa muziki wa hip hop 2Pac. Wimbo ulitolewa baada ya kufa kwake ikiwa na matoleo mawili mashuhuri yaliyotolewa kutoka katika albamu ya mwaka wa 2002, Better Dayz. Toleo la awali ili-rapiwa ikiwa na magitaa mawili ya akustika. Toleo lingine la akustika limemshirikisha rapa mwenzi-wake Nas na vilevile mwimbaji J. Phoenix. Ni wa pili kutoka katika wimbo wa mwisho wa kwenye Diski 1 ya Better Dayz. Toleo la remixi la "7", limemshirikisha mwimbaji Anthony Hamilton, ikiwa imeingizwa ukiwa wimbo wa 2 kwenye diski ya Better Dayz, ni wimbo pekee kutoka katika albamu kuwa na muziki wa video. Wimbo umeshika nafasi ya #19 kwenye chati za Billboard Hot 100. Toleo halisi la akustika pia linapatikana kwenye albamu ya Nas God's Son ikiwa chini ya jina la "Thugz Mansion (N.Y.)", ikiwa na mstari wa pili ulioimbwa na Tupac ikiwa inabadilishana-badilishana hadi kufikia kwenye mstari kamili wa Nas.

Thugz Mansion ulikuwa mfano wa 2Pac akiwa mbinguni. Wimbo huu ni mmoja kati ya nyimbo za 2Pac alizojichunguza na kujielezea kinafsi mno. Ndani ya wimbo huu, anazungumzia namna atakavyokufa na kupumzika kwa amani. Yaani, ya kwamba hatimaye amepata furaha pale akiwa katika sehemu ambapo matatizo yake na maumivu yake yamefikia kikomo. Na akisisitiza kusema kwamba ataishia mahala pa amani baada ya kufa kwake; pia ametaja majina kadhaa ya Waafrika-Waamerika mashuhuri (watu hao ni pamoja na: Marvin Gaye, Billie Holliday, Jackie Wilson, Sam Cooke, Malcolm X, Miles Davis) na tukio la kisiasa la hivi karibuni (yaani, Latasha Harlins), ambao wote katika hao anaamini ya kwamba wapo mbinguni.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Thugz Mansion" - 7" Remix (Explicit)
  2. "Thugz Mansion" - Nas Acoustic (Explicit)
  3. "F*ck Em All" (Explicit)
  4. "Thugz Mansion" - CD-ROM video