Nenda kwa yaliyomo

Soufiane Alloudi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Soufiane Alloudi

Soufiane Alloudi (سفيان علودي) (alizaliwa El Gara, 1 Julai 1983) ni mchezaji soka kutoka Moroko anayecheza kama mshambuliaji klabuni Kawkab de Marrakech.

Mwezi wa Tisa 2007, Alloudi alihamishiwa kutoka Raja Casablanca kwenda Al-Ain FC kwa mkataba wa miaka 3, na ada ya mkopo wake iliripotiwa kuwa dola 450,000.

Pia anachezea timu ya taifa ya Moroko, ambapo alifunga magoli matatu katika nusu ya kwanza ya mchezo katika dakika 28 dhidi ya Namibia katika mchezo wao wa ufunguzi wa 2008 Africa Cup of Nations. Alloudi aliondoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika kutokana na jeraha. Baada ya jeraha hilo, Moroko ilishindwa kufuzu robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na hivyo, kupoteza kwa Alloudi ilisemekana kuwa moja ya sababu za matokeo hayo.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Soufiane Alloudi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.