Shannon Boxx
Shannon Leigh Boxx Spearman ( née Boxx ; alizaliwa Juni 29, 1977) ni mchezaji wa soka mstaafu wa nchini Marekani na mwanachama wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya wanawake wa Amerika, akicheza nafasi ya kiungo. Mara ya mwisho alichezea klabu ya Chicago Red Stars katika Ligi ya Soka ya wanawake wa Amerika .
Alishinda medali za dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka 2004, Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, na Olimpiki ya London mwaka 2012. Pia alimaliza katika nafasi ya tatu akiwa na timu ya ya taifa ya Marekani katika Kombe la Dunia la FIFA la 2003, 2007, 2011 na 2015.
Alikuwa kwenye fainali ya tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wa FIFA mwaka 2005, na alishinda Mashindano ya Soka ya Wanawake ya NCAA na Notre Dame mnamo 1995. Shannon Boxx alitangaza kustaafu kutoka katika soka la kimataifa na klabu baada ya kushinda Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake lmwaka 2015 . Alicheza mchezo wake wa mwisho mnamo 21 Oktoba 2015 wakati USWNT ilipotoka sare na Brazil kama sehemu ya safari yao ya ushindi. [1]
Boxx ni dada mdogo wa Gillian Boxx, ambaye alishinda medali ya dhahabu katika Olimpiki ya 1996 akiwa na timu ya Marekani. [2]
Boxx aligunduliwa na ugonjwa wa lupus mnamo 2007 alipokuwa na umri wa miaka 30, na alitangaza utambuzi wake muda mfupi kabla ya Olimpiki ya London mwaka 2012 ambapo alishinda medali ya dhahabu akiwa na timu ya Marekani. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Bird, Liviu. "Shannon Boxx bids farewell as USWNT looks ahead to Rio with new players". Sports Illustrated. Iliwekwa mnamo Novemba 5, 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Shannon Boxx: USA's cool-headed heroine", FIFA.com, November 30, 2005. Retrieved on 2022-05-14. Archived from the original on 2008-01-17.
- ↑ "Olympic soccer player Shannon Boxx's battle with lupus", August 16, 2012.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shannon Boxx kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |