Rhodesia
Mandhari
Rhodesia ni jina la kihistoria kwa ajili ya maeneo ya nchi za kisasa Zimbabwe na Zambia wakati wa ukoloni kuanzia 1895.
Lamaanisha hasa nchi za
- Rhodesia ya Kusini (Zimbabwe) iliyojulikana kama "Rhodesia" tu kati ya 1964 na 1979 pia kama Zimbabwe-Rhodesia mwaka 1979 kabla ya kuitwa "Zimbabwe" pekee.
- Rhodesia ya Kaskazini iliyokuwa eneo lindwa la Uingereza na kupata uhuru wake kama "Zambia" mwaka 1964.
- Huko Uingereza kuna pia kijiji kinachoitwa "Rhodesia" katika wilaya ya Nottinghamshire takriban kilomita 30 kusini ya mji wa Sheffield. Haina uhusiano na historia ya jina la nchi za Afrika.