Pasha
Mandhari
Pasha | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 10:
|
Pasha ni ndege wadogo wa jenasi Malimbus katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika tu. Ndege hawa wana mwenendo kama kwera. Rangi zao ni nyeusi na nyekundu au nyeusi na njano. Hula wadudu hasa. Spishi hizi hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hayapatikani katika makundi makubwa kama yale ya kwera. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Malimbus ballmanni, Pasha wa Ballmann (Gola Malimbe)
- Malimbus cassini, Pasha Koo-jeusi (Cassin's Malimbe)
- Malimbus coronatus, Pasha Utosi-mwekundu (Red-crowned Malimbe)
- Malimbus erythrogaster, Pasha Tumbo-jekundu (Red-bellied Malimbe)
- Malimbus ibadanensis, Pasha wa Ibadan (Ibadan Malimbe)
- Malimbus malimbicus, Pasha Kishungi (Crested Malimbe)
- Malimbus nitens, Pasha Domo-buluu (Gray's or Blue-billed Malimbe)
- Malimbus racheliae, Pasha wa Rachel (Rachel's Malimbe)
- Malimbus rubricollis, Pasha Kitunga (Red-headed Malimbe)
- Malimbus scutatus, Pasha Tako-jekundu ( Red-vented Malimbe)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Pasha kishungi
-
Pasha domo-buluu