Palm Jumeirah
Palm Jumeirah ni kisiwa kilichoumbwa na binadamu kwa kutumia mtindo wa kurejesha ardhi na kampuni ya Nakheel, kampuni inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Ni moja ya visiwa vitatu viitwavyo Visiwa vya Palm ambavyo vimepanua ndani ya Ghuba ya Persia kuongeza pwani ya Dubai kwa jumla ya kilomita 520. Palm Jumeirah ni ndogo na Visiwa vitatu asili vya palm (Palm Jumeirah, Palm Jebel Ali na Palm Deira) yaliyojengwa na Nakheel. Iko katika eneo la pwani la Jumeirah la emirate ya Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Palm Jumeirah iko na sura ya mti wa mtende. Una shina, taji lililo na frond 16, na mpevu unaozunguka kisiwa ambao huunda kivunjamaji cha kilomita 11. Kisiwa ni kilomita 5 kwa kilometa 5 na jumla yake ni eneo kubwa kuliko nyanja 800 za mpira. Taji limeunganishwa na Bara na daraja la mita 300 na mpevu umeunganishwa na juu ya mitende na kishimo kilicho chini ya bahari [1] Katika miaka michache ijayo, kama awamu za utalii zinapoendelea, Palm Jumeirah inasemwa kuwa moja ya maeneo dunia's Premier Resorts. Kisiwa cha Palm kinajigamba kuwa shangazo ka nane la Dunia. Kisiwa kitaizidisha mara mbili urefu wa pwani ya Dubai. [2]
Kulingana na ujumbe wa vyombo vya habari kutoka kwa wajenzi,[3] kisiwa cha Palm cha Jumeirah kitakuwa na mahoteli ya kujirembesha yenye mandhari, aina tatu za nyumba za kifahari (Signature, Garden Homes na Canal Cove Town Homes), majengo ya ghorofa yaliyo kwenye pwani, fukwe, marinas, mikahawa, mikahawa midogo na aina nyingi za maduka ya rejareja. Mahoteli ya pwani zaidi ya 30 yatafunguliwa mwisho wa 2009 [1] yakiwemo:
- Rixos The Palm Dubai .
- Hoteli ya Trump International
- Atlantis, The Palm ilifunguliwa mwezi Septemba 2008.
- Hoteli ya Taj Exotica
- Makazi makubwa ya kifahari
- Jumba la Ottoman Linatumainiwa kuwa litafunguliwa mwisho wa 2009
- Essque Palm Jumeirah - Sehemu ya mradi wa Manyumba ya Tiara. Makao hayo yamepeanwa Hoteli itafunguliwa mwaka 2010.
- Oceana Resort & Spa
- Makao ya The Fairmount Palm
- Hoteli ya The Fairmount Palm
- Hifadhi na Hoteli ya Dubai Estates
- Hoteli ya Missoni Dubai
- Hoteli ya Radisson SAS Dubai , The Palm Jumeirah
- Jumba la Kempinski Emerald
- Makazi ya Kempinski Emerald Palace
Mandege mbili za vita za aina ya F-100 Super Sabre zimetolewa vitu vya ndani na kuzamishwa karibu na Palm Jumeirah ili kujenga reef ya bandia, lengo lake ni kutumiwa kama kivutio kwa waogeleaji
Tarehe 18 Juni 2007, kampuni ya Cunard Line ilitangaza kwamba ilikuwa ikiuza mashua yake ya kifahari ya zamani, RMS Queen Elizabeth 2 , kwa Istithmar kwa matumizi kama hoteli inayoelea katika Palm Jumeirah mwanzo wa mwaka 2009. [4] Hata hivyo, kama mwezi Julai 2009, inaonekana kama meli itahamishwa hadi Cape Town kwa matumizi katika maendeleo yasiyohusika na Nakheel [5]
-
Atlantis The Palm tarehe 21 Oktoba 2009, Hifadhi ya samaki ya The Lost Chambers
-
Atlantis The Palm tarehe 20 Novemba 2009, maoni kutoka kwa bahari kutoka kwa mpevu wa Palm, mbele ya Atlantis
Usafiri
[hariri | hariri chanzo]
Barabara ya kilomita 5.4 (maili 3.35) ya Palm Jumeirah Monorail, inayounganisha hoteli ya Atlantis na Gateway Towers ilifunguliwa 6 Mei mwaka 2009. [6]
Ujenzi
[hariri | hariri chanzo]Ujenzi ulianza mwezi Juni mwaka 2001 na wajenzi walitangaza makabidhiano ya vitengo vya makazi ya kwanza mwaka 2006 [1] Kisiwa kimeundwa na tani milioni 94 za mchanga na tani milioni 7 za mawe. Palm Jumeirah ilijengwa kwa kujaza mchanga kwenye kitanda cha bahari kilichi mita 10.5 chini ya maji kwa kutumia dredger. Juu ya bahari, mita 3 za ardhi iliyorejeshwa zilifikiwa kwa mtindo wa dredging unaojulikana kama "rainbowing" ambapo mchanga ulinyunyizwa kwenye kisiwa hicho. Mchanga wa aina ya Calcareous ulitumika kwa kurejesha ardhi. Kisiwa ni pamoja na kivunjamaji kilichojikunja kilichojengwa kwa kutumia kutumia mawe asili, lengo lake kuhimiza kuundwa kwa reef asili na kutoa makazi ya maisha ya bahari. Muundo huu wa arhi ulirejeshwa na kampuni ya Kiholanzi ya Van Oord, ambao ni wataalam duniani wa kurejesha ardhi. Jumla ya gharama ilifika US $ bilioni 12.3 na kudumisha kisiwa hicho inatumia gharama kubwa.i [onesha uthibitisho] Inakadiriwa wafanyakazi 40,000, wengi kutoka Asia ya Kusini, walishiriki katika ujenzi wa kisiwa.
Mapema Oktoba 2007, Palm Jumeirah tayari ilikuwa kisiwa kikubwa zaidi Duniani kilichoumbwa na mwanadamu. Pia wakati huu, asilimia 75 ya mali ilikuwa tayari kuuzwa, na tayari familia 500 zilikuwa zikiishi katika kisiwa hicho. [7] Mwisho wa 2009, hoteli 28 zitakuwa wazi katika mpevu. [7]
Ubishi
[hariri | hariri chanzo]Ukubwa wa ujenzi umelaumiwa, kwa sehemu sababu ya ucheleweshaji wa kukamilika kwa mradi, tarehe ambayo imesukumwa nyuma mara nyingi na sasa ni karibu miaka miwili kama imechelewa. Utata zaidi ulitokea pale ilipojulikana kwamba baada ya kuzindua mradi, Nakheel waliongeza idadi ya manyumba katika kisiwa (kwa kupunguza kiasi cha ardhi kati ya nyumba zile) kutoka kwa idadi iliyokuwa imetangazwa ya 4500 (ikiwa na manyumba 2000 ya kifahari na makazi 2500) hadi takriban manyumba 8000 bila kuwarudishia pesa wawekezaji ambao walikuwa wameyanunua manyumba hapo awali wakitegemea kuwa kutakuwa na utengaji zaidi kati ya manyumba. Ongezeko hili lilitokana na Nakheel kukosea katika kuhesabu gharama halisi ya ujenzi na kuhitaji pesa za ziada, ingawa hajawahi ongea kuhusu jambo hilo hadharani.
Wasiwasi pia umeonyeshwa kuhusu ubora wa ujenzi na uwezo wa kisiwa hiko kukabiliana na idadi ya watu watakaokuwa wakija na kuondoka kisiwani pale mradi utakapomalizika.
Aidha, kuna wasiwasi mwingi kuhusu madhara ya mazingira ya Kisiwa hiki. Kama ilivyojengwa awali,kivunjamaji kilikuwa kikwazo mfululizo, lakini iligunduliwa kwamba kwa kuyazuia maji ya pale kusonga, maji ya ndani ya Palm yalibakia palepale. Tatizo lilitatuliwa kwa kuongeza pengo katika kizuizi. [8] Kama ilivyoelezwa katika kipindi cha National Geographic Channel cha Impossible Islands sehemu ya mfululizo wake wa MegaStructures, kizuizi hiki kilibadilishwa baadaye ili kuweka pengo katika pande zote mbili, ili kuyawezesha maji ya baharini kuongeza hewa katika maje ya pale ndani ingawa haingekuwa na ufanisi ukilinganisha na kama kizuizi hakingekuwepo. Kipindi hiki pia kilitaja kuhusu maisha ya baharini, lakini kilisema kuea kizuizi hiki kiliimarisha maisha ya baharini na aina mpya za maisha ya baharini zilikuwa zikihamia pale.
Katika makala ya 2009 iliyoelezea kuanguka kwa uchumi wa Dubai, The New York Times iliripoti kwamba "fununu mbaya" zilikuwa zikienea kwamba Palm ilikuwa ikizama "na ukifungua mifereji katika hoteli zilizojengwa yake, mende tu ndizo zilitoka nje." [9]
Hifadhi ya Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Majumba ya Kifahari yaliyo katika mgawanyiko mmoja (Frond)
-
Migawanyiko ya Palm Jumeirah
-
Maoni ya hewani ya Palm Jumeirah tarehe 1 Mei 2007
-
Maoni ya hewani ya Palm Jumeirah tarehe 1 Mei 2007
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2
{{cite web}}
: Empty citation (help) - ↑ "Pitfalls in paradise: why Palm Jumeirah is struggling to live up to the hype". guardian.co.uk. 2008-04-26. Iliwekwa mnamo 2008-04-27.
- ↑ "The Palm Jumeirah". Nakheel Website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-09. Iliwekwa mnamo 2007-06-19.
- ↑ "QE2 To Leave Cunard Fleet And Be Sold To Dubai World To Begin A New Life At The Palm". [1]. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-06. Iliwekwa mnamo 2007-06-20.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); External link in
(help)|publisher=
- ↑ "QE2 Today: The Future". [2]. 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-19. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); External link in
(help)|publisher=
- ↑ http://www.khaleejtimes.com/DisplayArticle.asp?xfile=data/theuae/2009/May/theuae_May169.xml§ion=theuae&col Archived 20 Januari 2015 at the Wayback Machine. =
- ↑ 7.0 7.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedProgress Update
- ↑ "Palm Island Dubai FAQ".
- ↑ [38] ^ Watalii waliotulia watoroka baada ya Dubai kuanza kuanguka, New York Times, 11 Februari 2009
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Rasmi ya Palm Jumeirah Archived 10 Februari 2012 at the Wayback Machine.