Nenda kwa yaliyomo

Pal Engjëlli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pal Engjëlli (1416–1470) alikuwa kardinali wa Kanisa Katoliki, msomi, na Askofu Mkuu wa Durazzo (sasa Durrës, Albania).

Mnamo mwaka 1462, aliandika sentensi ya kwanza inayojulikana hadi sasa kwa lugha ya Kialbania.

Alitoka katika familia ya Engjëlli, akiwa mtoto wa Andrea Engjëlli na Dorothea Arianiti. Pal Engjëlli alihusiana kwa karibu na Skanderbeg, akihudumu kama rafiki, mshauri na mjumbe wake katika safari mbalimbali za kidiplomasia kutafuta msaada wa kupambana na Milki ya Ottoman.

Alifanikiwa kumshawishi Dukagjinii Lekë kuachana na Waturuki wa Ottoman na baadaye kupatana na Skanderbeg. Pia alimshawishi Skanderbeg kuvunja mkataba wa amani aliokuwa ameusaini na Waturuki.[1]

Dirisha la kisasa la vioo la Pal Engjëlli (katikati na mavazi meusi).
  1. Božić, Ivan (1979), Nemirno pomorje XV veka (kwa Kiserbia), Beograd: Srpska književna zadruga, uk. 380, OCLC 5845972, захваљујући помоћи драчког архиепископа Павла Анђела, који је успео да одвоји Леку од Турака и доцније измири са Скендербегом, а исто тако и да Скендербега наведе на прекид примирја са Турцима
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.