Nyoka Meno-hanjari
Mandhari
Nyoka meno-hanjari | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
|
Nyoka meno-hanjari ni spishi ya nyoka wa jenasi Xyelodontophis katika familia Colubridae. Amepewa jina hili kwa sababu ana chonge ndefu zinazofanana na hanjari.
Nyoka huyu ni warefu kiasi: m 1-1.5. Rangi yake ya juu ni kijivu au kahawia pamoja na vidoa njano. Taya la chini ni jeupe, koo njano na tumbo jeusi.
Makazi na mwenendo haijulikani vizuri lakini sampuli moja ilipatikana yenye kinyonga ndani ya tumbo lake.
Chonge ni meno marefu ya nyuma yanayofanana na hanjari. Haijulikani kama sumu ni hatari.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka Meno-hanjari kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |