Nenda kwa yaliyomo

Novatus Dismas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Novatus Dismas Miroshi
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 2 Septemba 2002
Mahala pa kuzaliwa    Tanzania
Nafasi anayochezea Kiungo wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Shaktar Donesk
Timu ya taifa
Timu ya Taifa ya Tanzania

* Magoli alioshinda

Novatus Dismas Miroshi (alizaliwa 2 Septemba 2002) ni mchezaji wa soka wa nchini Tanzania ambaye kwa sasa anachezea katika klabu ya Gotzepe ya uturuki na Timu ya Taifa ya Tanzania.

Novatus alianza maisha yake ya mpira kweny club ya azam football club ya nchini Tanzania akianzia timu za vijana kabla ya kupandishwa kwenda timu ya wakubwa ambapo hakufanya vizuri na akatolewa kwa mkopo kwenda timu ya biashara united ya Musoma mkoani Mara ambapo alifanya vizuri sana na kua mchezaji bora chipukizi [1]

Baada ya kufanya vizuri akiwa na biashara united alijiunga na club ya maccabi Tel Aviv ya Israel.

Mnamo mwaka 2022, Dismas alisaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya SV. Zulte Waregem huko Ubelgiji.[2]

Ushiriki Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Dismas alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa katika timu ya taifa ya soka ya Tanzania chini ya miaka 20 mnamo 16 Februari 2021 katika mchezo wa mechi ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika U-20 ambapo timu ya taifa ya soka ya Ghana chini ya miaka 20 ilishindwa kwa mabao 4-0. Mnamo 19 Februari, alifunga bao lake la kwanza kwa katika timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya timu ya taifa ya soka ya chini ya miaka 20 ya Gambia katika mechi iliyotoka sare kwa bao 1 - 1.

Mnamo 2 Septemba 2021, Dismas alicheza katika mechi ya timu ya taifa ya soka ya Tanzania katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya soka ya DR Congo katika mechi ya kufuzu ya Kombe la Dunia 2022.[3] Mnamo 7 Septemba, alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 3 - 2 dhidi ya timu ya taifa ya soka ya Madagaska.[4]

  1. "Google". www.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-12-23.
  2. "Novatus Miroshi is trots om boer te zijn" (kwa Kiholanzi). Zulte Waregem. 22 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "FIFA". fifa.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  4. "FIFA". fifa.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Novatus Dismas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.