Ndoero
Mandhari
Ndoero | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Ndoero ni ndege wa jenasi Dromas, jenasi pekee ya familia Dromadidae. Spishi hii inafanana na kiluwiluwi mwenye miguu mirefu lakini ina domo refu na nene. Rangi zake ni nyeupe na nyeusi. Hula kaa, kombe na makoa ya bahari. Ndege hawa hupenda kuzaa katika makoloni ya ndege wengi, hadi 1500. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga. Jike hulitaga yai moja jeupe tu, pengine mayai mawili. Tofauti na viluwiluwi kinda la ndoero hatembei sasa hivi akitoka yai.
Nasaba za ndoero hazielei. Wataalamu wengine hufikiri kwamba spishi hii ina mnasaba na chekehukwa au bwabwaja, wengine hufikiri kwamba ina mnasaba zaidi na alka na shakwe.