Nenda kwa yaliyomo

Mtapo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtapo wa chuma
Madini ya magnetiti (oksidi ya chuma) katika mtapo

Mtapo (wakati mwingine pia mbale[1]; kwa Kiingereza: ore) ni mwamba asilia au mashapo yenye madini ya thamani ndani yake, hasa yenye metali ndani yake.

Mtapo hupatikana katika ardhi au chini ya ardhi au ndani ya mlima ukitolewa kwa kuuchimba, mara nyingi katika migodi. Hapo mtapo unapondwa na sehemu kubwa ya ardhi au miamba isiyo na tija hupunguzwa kwa mbinu mbalimbali.Tokeo lake ni makanikia (ore conventrate) yenye kiwango kikubwa cha madini yanayotafutwa. Yanatolewa katika makanikiakwa njia mbalimbali za kuusafisha, kwa mfano kwa kuupasha moto hadi metali ndani yake inayeyuka, au kwa njia za kemikali zinazounda kampaundi na madini inayotafutwa; kampaundi hiyo inasafishwa baadaye tena.

Thamani ya mtapo hutegemea kiwango cha madini yanayotafutwa ndani wake. Hii inategemea na maendeleo ya tekinolojia na bei ya madini yenyewe kwa upande mmoja na gharama za kutoa mtapo ardhini na kuusafisha kwa upande mwingine.

Madini ambayo mitapo yake hupatikana kwa umbo la oksidi, sulfidi na silikati au tayari kama metali kama vile shaba na dhahabu. Kwa mfano chuma hupatikana kiasili zaidi kama oksidi za Fe3O4 (magnetiti) na Fe2O3 (hematiti).

  1. Kamusi Kuu ya BAKITA, KKS na KKK/SED ya TUKI na Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia hutumia "mtapo", ilhali KKK/ESD ya Tuki inatumia "mbale", inayotumika pia katika maandiko ya Wizara ya Madini Tanzania (Mfano uk. 6 Archived 25 Oktoba 2020 at the Wayback Machine..
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.