Nenda kwa yaliyomo

Mexico (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Mexico
Jiji la Mexico is located in Mexiko
Jiji la Mexico
Jiji la Mexico

Mahali pa mji wa Mexico katika Mexico

Majiranukta: 19°26′0″N 99°8′0″W / 19.43333°N 99.13333°W / 19.43333; -99.13333
Nchi Mexiko
Tovuti:  http://www.df.gob.mx/
Mexico
Nembo ya Jiji la Mexiko tangu mwaka 1523.

Jiji la Mexico (kwa Kihispania: Ciudad de México) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa nchi ya Mexico. Jiji lina wilaya 16, ambazo kila moja zimegawanywa katika vitongoji au colonias.

Uko kwenye nyanda za juu za Mexico kwenye kimo cha m 2000 juu ya UB katika bonde refu linalopakana na milima mirefu. Kati ya milima hii ni volkeno za Popocatepetl na Iztaccihuatl na nyororo ya Sierra Nevada.

Mji wa Mexico ni pia mkoa wa kujitegemea, huitwa mara nyingi na Wamexiko wenyewe "Mexico DF" au kwa kifupi "DF" (DF = Distrito Federal, Mkoa wa Shirikisho), lakini tangu mwaka 2016 unaelekea kujitegemea zaidi kiutawala.

Idadi ya wakazi ni milioni 9, lakini pamoja na mitaa ya karibu idadi inafikia karibu milioni 20.4. Ni kati ya miji mikubwa kabisa duniani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya mji ilianza mwaka 1325. Wakati ule kikosi cha Azteki wahamiaji walifika kwenye ziwa la Texcoco na kujenga makao kwenye kisiwa ziwani wakauita mji "Tenochtitlan".

Kuna hadithi ya kale juu ya kuundwa kwa Tenochtitlan ambao ni mji wa Kiazteki uliotangulia Mexiko City.

Zamani ile Waazteki waliishi maisha ya kuhamahama na kutafuta mahali pa kujenga mji wa kudumu. Mungu wao Huitzilopochtli aliwaambia wamtafute anayekalia mpungate (kakati) na kushika nyoka. Mpungate utapatikana kwenye mwamba katika kisiwa ziwani. Hadithi yaendelea kusema ya kwamba baada ya matembezi ya miaka 200 walikuta ziwa la Texcoco penye mwamba na mpungate. Walipokaribia tai aliyeshika nyoka akaketi kenye mpungate huu.

Baada ya kupokea ishara hiyo waliunda mji wao wa Tenochtitlan uliokuwa baadaye mji mkuu wa Dola la Azteki. Ulikuwa na wakazi 300,000 wakati wa kufika kwa Wahispania mwaka 1519.

Mwaka 1519 alifika Mhispania Hernan Cortez pamoja na jeshi la askari 450. Baada ya kupokewa vizuri na mfalme wa Azteki Montezuma walimkamata kama mfungwa na kuchukua dhahabu kutoka mahekalu.

Wenyeji wa mji waliwashambulia na kuua Wahispania wengi. Cortes aliweza kukimbia akarudi na jeshi jipya akaweza kuteka mji tarehe 13 Agosti 1521 na kuuharibu kabisa.

Mji wa Mexico

[hariri | hariri chanzo]

Wahispania walianzisha mji mpya juu ya maghofu ya mji wa kale. Makanisa yalijengwa mahali pa mahekalu ya kale.

Tangu mwaka 1525 mji wa Mexiko ulikuwa mahali pa serikali ya nchi, tangu 1535 mji mkuu wa "Ufalme Mdogo wa Hispania Mpya". Makoloni ya Hispania ya Guatemala, Kuba, Florida na hata Ufilipino katika Asia yalitawaliwa kutoka hapa.

Mji ulikuwa mji mkuuwa wa nchi huru tangu 1821.

Katika karne ya 20 ilikua haraka sana.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mexico (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.