Nenda kwa yaliyomo

Mchikichi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchikichi
(Elaeis guineensis)
Mchikichi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Arecales (Mimea kama mpopoo)
Familia: Arecaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mpopoo)
Jenasi: Elaeis
Spishi: Elaeis guineensis Jacq.

Elaeis oleifera (Kunth) Cortés

Mchikichi (Elaeis guineensis) ni kati ya miti iliyo muhimu zaidi kiuchumi. Matunda yake huleta mawese ambayo hutumika sana kama mafuta ya kupikia, kwa ajili ya madawa mbalimbali na siku hizi pia kama diseli.

Mti unakua hadi kimo cha m. 30. Matunda yake ni madogo yakiwa pamoja kwa shingo. Jumla ya mti mmoja laweza kufikia 50 KG. Matunda haya huharibika haraka hivyo ni muhimu kuyashughulika mara moja baada ya mavuno.

Asili yake Mchikichi ni Afrika ya Magharibi. Mti huu ulipewa jina la kisayansi "Elaeis guenesis" kwa sababu kiasili ilipatikana kwa wingi katika nchi za kanda ya Guinea. Siku hizi inakuzwa zaidi katika Amerika na hasa Asia ya kusini.

Nchi asilia za mchikichi

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ukoloni michikichi ilipatikana katika kanda ya kitropiki ya Afrika.

Kwanza katika nchi za kanda ya Guinea: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Benin, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Togo.

Lakini imepatikana pia Afrika ya Mashariki: Kenya, Tanzania, Uganda.

Migunda ya michikichi

[hariri | hariri chanzo]

Migunda mikubwa ya michikichi iko hasa Malaysia na Indonesia zenye mavuno ya 80% ya mawese duniani.

Brazil na Kolumbia ziemanza vilevile kupanda michikichi kwa wingi.

Uthai, Papua–Guinea Mpya na nchi za Afrika ya Magharibi zinachangia asilimia ndogo kwenye soko la dunia ya mawese. Katika Afrika kuna migunda mikubwa kidogo huko Nigeria, Côte d'Ivoire, Kamerun na Kongo Kinshasa.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]