Mauzo
Mauzo ni shughuli inayohusiana na kuuza au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa katika muda fulani.
Muuzaji humaliza kitendo cha uuzaji baada ya kujibu mwito wa ununuzi. Kuna kupitisha umiliki wa bidhaa na kulipa, ambapo kuna makubaliano ya bei ambayo italipiwa bidhaa ile. Muuzaji ndiye anayefanya tendo lile la uuzaji na uzo lile linaweza kumalizika kabla ya mnunuzi kumaliza kulipa.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Mtu au shirika linaloonyesha nia ya kupata bidhaa ya thamani inayotolewa linajulikana kama mnunuzi au mteja mtarajiwa. Kununua na kuuza ni lile tendo la kubadilishana umiliki. Kununua ni kupokea umiliki wa kinachouzwa ilhali kuuza ni kupitisha umiliki kwa mnunuzi baada ya malipo. Muuzaji na mnunuzi huafikiana ili kukamilisha ubadilishaji wa thamani.[1]
Katika mauzo kunaweza kuwa na kujadiliana bei au bei inaweza kuwa isiyobadilika. Sanasana bei ya bidhaa au huduma hukuliwa na haja ya wanunuzi na wingi wake sokoni. Kwa biashara zinazolenga wanunuzi fulani, hasa matajiri, muuzaji anaweza kuiweka bei ya bidhaa bila kuzingatia bei ya ile bidhaa au huduma sokoni.
Mbinu
[hariri | hariri chanzo]Mauzo yanaweza kuwa:[2]
- Ya moja kwa moja
- Yasiyo ya moja kwa moja
- Ya kupitia mawakala
- Ya rejareja
- Ombi la pendekezo
- Biashara kwa biashara[3]
- Ya kielektroniki
Mawakala wa mauzo
[hariri | hariri chanzo]Mawakala katika mchakato wa mauzo wanaweza kuwakilisha upande wowote; kwa mfano:
- Wakala wa mauzo (kama vile kupitia mauzo shirikishi)
- Wakala mnunuzi
- Wakala anayewakilisha pande zote mbili
- Wakala wa kuangalia shughuli tu
- Uwakilishi wa nje wa mambo ya mauzo
- Msimamizi wa mauzo wa kutekeleza mikakati ya mauzo na kuratibu idara ya mauzo
- Mfanyabiashara muuzaji
- Wataalamu wa mauzo mtandaoni
Aina za uuzaji
[hariri | hariri chanzo]- uso kwa uso (P2P)
- uso kwa biashara (P2B)
- biashara kwa biashara (B2B)
Aina za mauzo kijiografia
[hariri | hariri chanzo]- mauzo ya ndani
- mauzo ya serikali
- mauzo ya nchi
- mauzo ya kimataifa[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Putthiwanit, C.; Ho, S.-H. (2011). "Buyer Success and Failure in Bargaining and Its Consequences". Australian Journal of Business and Management Research. 1 (5): 83–92.
- ↑ Compendium of Professional Selling. United Professional Sales Association. n.d. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-26. Iliwekwa mnamo 2017-12-02. Archived 26 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- ↑ John, Bryson (10 Feb 2003). "What To Do When Stakeholders Matter: A Guide to Stakeholder Identification and Analysis Techniques" (PDF). London School of Economics and Political Science.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adam Rosen (lead Financial Writer) "Professional sales Analysis". Professional sales. Iliwekwa mnamo 2011-02-14.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mauzo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |