Nenda kwa yaliyomo

Martino wa Tours

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Martino akimgawia maskini nusu ya koti lake. Höchster Schloss, Höchst (Frankfurt am Main), Ujerumani.
"Upendo wa Mt. Martino" ulivyochorwa na Jean Fouquet.
Mt. Martino na Ombaomba, walivyochorwa na El Greco, 1597-1599 hivi (National Gallery of Art, Washington).
Mt. Martino akiacha jeshi alivyochorwa ukutani na Simone Martini.
Basilika la Mt. Martino, Tours.

Martino wa Tours (Savaria, Panonia, leo Hungaria 316 - Candes-Saint-Martin, Gaul, leo Ufaransa 397) alikuwa mmonaki, halafu askofu (kuanzia 371 hadi kifo chake).

Kisha kuzaliwa na Wapagani, aliitwa jeshini sehemu za Ufaransa. Huko, akiwa bado mkatekumeni, alimfunika kwa joho lake Kristo aliyetwaa sura ya fukara.

Baada ya kubatizwa, aliacha jeshi na kuishi kitawa huko Ligugé katika monasteri aliyoianzisha mwenyewe, akiwa chini ya uongozi wa Hilari wa Poitiers.

Hatimaye alipewa daraja takatifu ya upadri akachaguliwa kuwa askofu wa Tours, akawa mfano wa Mchungaji mwema, akianzisha monasteri nyingine na parokia vijijini, akifundisha na kupatanisha waklero na kuinjilisha wakulima hadi mwisho kabisa wa maisha yake [1].

Alipokaribia kifo, walimuomba asiondoke, naye akasali hivi: "Ee Bwana, nikihitajiwa bado na watu wako, sikatai uchovu wa kazi: utakalo lifanyike!"

Maisha yake yaliandikwa na Sulpicius Severus yakawa kielelezo cha vitabu juu ya watakatifu.

Sifa yake ilienea haraka hivi kwamba aliheshimiwa kama mtakatifu ingawa hakuwa mfiadini kama kawaida ya wakati ule. Hadi leo anaheshimiwa hivyo na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri n.k.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 11 Novemba[2], ila kwa Waorthodoksi tarehe 11 Oktoba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Sulpicius Severus On the Life of St. Martin. Translation and Notes by Alexander Roberts. In A Select Library of Nicene and Post-Nicene Fathers of the Christian Church, New York, 1894, available online Ilihifadhiwa 2 Machi 2018 kwenye Wayback Machine.
  • Clare Stancliffe, St Martin and his hagiographer: History and miracle in Sulpicius Severus (Oxford, Clarendon Press, 1983), pp. xvi+400 (Oxford Historical Monographs).
  • Mark Kurlansky (2006). Nonviolence: twenty-five lessons from the history of a dangerous idea. Modern Library chronicles book, Random House, Inc., New York. ISBN 0-679-64335-4.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.