Kiwalani
Kata ya Kiwalani | |
Mahali pa Kiwalani katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°49′26″S 39°14′56″E / 6.82389°S 39.24889°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Dar es Salaam |
Wilaya | Ilala |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 40,049 |
Kiwalani ni mojawapo kati ya kata zilizopo katika wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, nchini Tanzania, yenye postikodi namba 12108. Iko ndani ya jiji la Dar es Salaam na kupakana na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Kwa upande wa mashariki imepakana na barabara ya Nyerere, upande wa kusini imepakana na kituo cha reli ya TAZARA.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 40,049 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kitongoji kilikuwa na idadi ya wakazi wapatao 82,292.[2]
Kitongoji hiki kilianzishwa miaka ya 1970 baada ya watu kuhamishwa na serikali kutoka katika viwanja vyao sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
Mgawanyiko wa Kiwalani
[hariri | hariri chanzo]Kiwalani ina mgawanyiko mkubwa sana, pia ina majina tofauti mengi tu, kama:
- Kiwalani Kariagogo
- Kiwalani Minazi Mirefu
- Kiwalani Bombom
- Kiwalani Kigilagila
- Kiwalani Yombo
- Kiwalani Deimasoko
Kwa upande wa Bombom, kidogo eneo lake limekaa vyema kwa kutokuwa na madimbwi mengi ya maji jinsi ilivyo upande wa Kiwalani Kigilagila. Kigilagila kuna maji mengi mno - hasa kipindi cha masika kuna hali mbaya kupita kiasi. Wakazi wengi wanaokalia maeneo ya shule ya msingi ya Kiwalani huwa tabuni kwa kipindi hicho: madimbwi, mitaro mibovu, mashimo yasiyo na mpangilio na upangiliaji usiofaa wa makazi ya watu. Kiwalani Minazi Mirefu kupo sawa na na Kijiwe Samli kwa sababu kumeinuka hivyo maji hayakai sana kama jinsi ilivyo kwa upande wa Kigilagila.
Deimasoko napo kunafanana kabisa na mfumo mpangilio mbovu wa makazi. Yaani, kupo hovyohovyo - kiasi kwamba nyumba zimebanana hadi kero. Madimbwi ya maji ni mengi mno kupita kiasi. Eneo hili malaria huwa juu sana kutokana na madimbwi yaliyopo huko. Kinachosabisha eneo la Kigiglagila kuwe na maji mengi, ni kwa sababu eneo la kule lilikuwa eneo la mashamba ya mpunga. Kwa namna moja au nyingine, Kiwalani yote lilikuwa eneo la mashamba ya mpunga. Ndiyo maana kila eneo lake limetapakaa majimaji.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz/
- ↑ "Sensa ya 2012, Kiwalani" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-08-18.
Kata za Wilaya ya Ilala - Tanzania | ||
---|---|---|
Bonyokwa | Buguruni | Buyuni | Chanika | Gerezani | Gongolamboto | Ilala | Jangwani | Kariakoo | Kimanga | Kinyerezi | Kipawa | Kipunguni | Kisukuru | Kisutu | Kitunda | Kivukoni | Kivule | Kiwalani | Liwiti | Majohe | Mchafukoge | Mchikichini | Minazi Mirefu | Mnyamani | Msongola | Mzinga | Pugu | Pugu Station | Segerea | Tabata | Ukonga | Upanga Magharibi | Upanga Mashariki | Vingunguti | Zingiziwa |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kiwalani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |