Kitale
Mandhari
Kitale | |
Mahali pa mji wa Kitale katika Kenya |
|
Majiranukta: 1°01′0″N 35°0′0″E / 1.01667°N 35.00000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Trans-Nzoia |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 106,187 |
Kitale ni mji wa Kenya katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Ni makao makuu ya kaunti ya Trans-Nzoia.
Mji uko mita 1900 juu ya usawa wa bahari.
Hifadhi ya Taifa ya Saiwa Swamp iko karibu na mji, ambao unajulikana pia kwa makumbusho ya Kitale [1].
Mazao ya sokoni inayokuzwa katika sehemu hii ni majani ya chai, kahawa, pareto, alizeti, maharagwe na mahindi. Kitale ni soko la mazao ya kilimo na kituo cha kilimo cha mseto.
Mji huu ulianzishwa mwaka wa 1908 na Wazungu walowezi. Reli ya Uganda kutoka Eldoret ilifika Kitale mwaka wa 1926 na ilichangia kukuza mji huu. Kadiri ya sensa ya mwaka 2009, mji ulikuwa na wakazi 106,187[2].
Tazama pia
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-11. Iliwekwa mnamo 2010-08-29.
- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Viungo vya nje
- ramani-mwiinuko =mita 1896 (alama nyekundu ni reli)
- manispaa ya Kitale Archived 31 Mei 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kitale kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |