Nenda kwa yaliyomo

Haji Mnoga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Haji Mnoga
Maelezo binafsi
Jina kamiliHaji Suleiman Haji Mnoga
tarehe ya kuzaliwa16 Aprili 2002 (2002-04-16) (umri 22)
mahali pa kuzaliwaPortsmouth, Uingereza
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasaSalford City
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2008-2024Portsmouth5(0)
2019Bognor Regis Town (mkopo)1(0)
2021Bromley (mkopo)6(0)
2022Weymouth (mkopo)19(0)
2022Gillingham (mkopo)4(0)
2023Aldershot Town (mkopo)17(1)
2023-2024Aldershot Town (mkopo)33(2)
2024 -Salford City (mkopo)7(0)
Timu ya Taifa ya Kandanda
Tanzania8(0)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 121 April 2024

Haji Suleiman Haji Ali Mnoga (alizaliwa Portsmouth, 16 Aprili 2002) ni mchezaji wa kimataifa wa mpira wa miguu anayecheza nafasi ya Mlinzi wa kulia kwenye klabu ya Salford City F.C. ya nchini Uingereza.

Ingawa ni mzaliwa wa Uingereza, anaitumikia timu ya Taifa ya Tanzania.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Haji Mnoga alizaliwa na baba raia wa Tanzania huku mama yake akiwa Mwingereza. Mnoga alisoma shule ya msingi Trafalgar. Baba yake alishawahi kucheza mpira pia, alichezea timu ya taifa ya Zanzibar kwa wachezaji chini ya miaka 17.

Kazi Ngazi ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzo mwa maisha ya soka, Mnoga alikulia katika klabu ya Portsmouth F.C. Amecheza katika klabu hiyo kuanzia mwaka 2008. Mnamo Juni 28, 2018, alisaini mkataba wa miaka miwili wa ufadhili wa masomo yake.[1]

Mnoga alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimashindano tarehe 9 Oktoba 2018, alianza kwenye kikosi cha kwanza na walishinda kwa goli 1–0 dhidi ya mpinzani wao klabu ya Crawley Town F.C. Mchezo huo ulikua ni katika mashindano ya Kombe la EFL.[2] Akiwa na miaka 16, miezi mitano na siku 24, aliweka historia ya kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo kuwahi kucheza katika klabu hii, aliyeshikilia nafasi ya kwanza ni mchezaji mwenzake kutoka timu ya vijana Joe Hancott.

Mnamo Machi 20, 2020, Mnoga alipata maambukizi ya virusi vya Corona.[3]

Mnoga alipona Septemba 2020, na aliweza kucheza kwenye mechi ya maandalizi ya msimu akiwa na klabu ya Gosport Borough F.C. walishinda 1-0 mpinzani akiwa ni klabu ya Havant & Waterlooville F.C., mchezo huu ulichezwa katika uwanja wa Privett Park. Mnoga alicheza mchezo huu kwa mkopo wa jioni hiyo tu akitokea Portsmouth, klabu hizi mbili ni majirani kabisa, wakiwa wametenganishwa na bandari.

Mnamo 3 Novemba 2020, Mnoga alicheza mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu ya Portsmouth, alianza mchezo huu kama mchezaji wa akiba, alipoingia alicheza nafasi ya winga wa kulia na walishinda mchezo huo kwa magoli 3-1 dhidi ya Lincoln City F.C.[4] Mchezo wake wa kwanza kwenye ligi alicheza dhidi ya Crewe Alexandra, mchezo huo alianzia nje, na aliingia mwanzoni mwa kipindi cha pili, walishinda mchezo huo kwa magoli 4-1. Mnamo Disemba 8, 2020, alifunga goli lake la kwanza, hii ilikua ni kwenye mashindano ya Kombe la EFL dhidi ya Cheltenham Town F.C, mchezo hup uliisha sare.[5] Agosti 31 2021, Mnoga alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu kwenye klabu ya Portsmouth, hii ni kabla ya kuhamia kwa mkopo kwenye klabu ya Bromley inayoshiriki daraja la tano katika mpangilio wa ligi nchini Uingereza, alibaki Bromley hadi Januari 2022.[6]

Januari 8 2022, Mnoga alihamia klabu ya Weymouth kwa mkopo na kusalia hapo kwa msimu wote wa 2021-22.[7] Siku ya mwisho ya kipindi cha uhamisho ya majira ya joto yam waka 2022, alijiunga na Gillingham F.C kwa mkopo wa muda mrefu,[8] kwenye mchezo wake wa kwanza, alitolewa kwenye mchezo katika dakika ya kumi tu.[9] Alijiunga na Aldershot Town F.C kwa mkopo Januari 2023 na kusalia klabuni hapo mpaka misho wa msimu.[10]

Ilipofika Agosti 2 2023, Mnoga alirudi kwa mara nyingine kwenye klabu ya Aldershot akwa mkopo wa msimu mzima.[11]

Tarehe 1 Mei 2024, Portsmouth waliweka wazi kuwa wataachana na Mnoga mkataba wake utakapofikia tamati majira ya Joto.[12]

Mnoga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Salford City F.C inayoshiki ligi daraja la pili tarehe 30 Agosti 2024.[13]

Kazi Ngazi ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Mnoga alifdanikiwa kuziwakilisha Uingereza na Tanzania katika michezo ya kimataifa. Mnamo Februari 10 2019, alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye Timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 17, aliingia kipindi cha pili akitokea benchi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Hungary ambapo walishinda 4-1 kwa mikwaju ya penati.[14] Alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Timu ya Taifa ya Tanzania tarehe 24 Machi 2022 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na walishinda magoli 3-1.[15] Iliripotiwa kwamba Mnoga alikataa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 alipochaguliwa Septemba 2022, sababu ikiwa ni kutaka kuzingatia majukumu yakwe kwenye klabu ya Gillingham.[16]

As of Oktoba 12 2024[17]
Michezo na magoli ngazi ya Klabu, misimu na mashindano
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Ligi ya EFL Mengine Jumla
Ngazi Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli
Portsmouth F.C. Msimu : 2018–19 Ligi ya EFL 0 0 0 0 0 0 3Kigezo:Efn 0 3 0
Portsmouth F.C. Msimu: 2019–20 0 0 0 0 0 0 1Kigezo:Efn 0 1 0
Portsmouth F.C. Msimu: 2020–21 5 0 1 0 0 0 3Kigezo:Efn 1 9 1
Portsmouth F.C. Msimu: 2021–22 0 0 0 0 0 0 2Kigezo:Efn 0 2 0
Portsmouth F.C. Msimu: 2022–23 0 0 0 0 2 0 1Kigezo:Efn 0 3 0
Portsmouth F.C. Msimu: 2023–24 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
Jumla 5 0 1 0 2 0 10 1 18 1
Bognor Regis Town (mkopo) Ligi ya Isthmian: 2019–20 Ligi kuu ya Isthmian 1 0 0 0 0 0 1 0
Bromley F.C. (mkopo) National League: 2021–22 National League 6 0 1 0 0 0 7 0
Weymouth F.C. (Mkopo) National League: 2021–22 National League 19 0 0 0 1Kigezo:Efn 0 20 0
Gillingham F.C. (Mkopo) Gillingham F.C. Msimu: 2022–23 EFL League Two 4 0 1 0 0 0 0 0 5 0
Aldershot Town (loan) National League: 2022–23 National League 17 1 0 0 2Kigezo:Efn 0 19 1
National League: 2023–24 National League 33 2 3 0 1Kigezo:Efn 0 37 2
Jumla 50 3 3 0 0 0 3 0 56 3
Salford City F.C. Salford City F.C. Msimu: 2024–25 Ligi Daraja la Pili EFL 7 0 0 0 0 0 1Kigezo:Efn 0 8 0
Jumla Ya magoli 92 3 6 0 2 0 15 1 115 4

Portsmouth

  • Kombe la EFL: 2018–19


  1. "Blues Sign Eight New Apprentices". Portsmouth FC. 28 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Crawley 0 Pompey 1". Portsmouth F.C. 9 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Haji Mnoga the fourth Portsmouth player to test positive for coronavirus", portsmouth, 21 March 2020. Retrieved on 21 March 2020. 
  4. "The Football League debut which franked all the recent Portsmouth soundbites". Portsmouth News. 4 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Cheltenham 0 Portsmouth 3 - England eyes on impressive Haji Mnoga after inspiring Blues to Papa John's Trophy He also played for guernsey Fc between February 2024 and summer 2025 before barnsley bought him for 215k when he was going to be the famous scott williams' replacement at centre back.progress". portsmouth.co.uk. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Mnoga Pens New Contract". Portsmouth FC. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Haji Mnoga is a Terra!". Weymouth FC. 8 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Haji Mnoga signs for Gills on loan". Gillingham FC. 2 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Gillingham v Swindon Town". BBC Website. 3 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "NEW SIGNING: Haji Mnoga". www.theshots.co.uk. 17 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "NEW SIGNING: Haji Mnoga". www.theshots.co.uk. 2 Agosti 2023. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Pompey Retained List: Summer 2024". www.portsmouthfc.co.uk (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-05-01.
  13. FC, Salford City (2024-08-30). "International defender signs one-year deal". Salford City FC (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-10-12.
  14. "Portsmouth defender makes debut for England under-17s". Portsmouth News. 11 Februari 2019. Iliwekwa mnamo 11 Februari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Taifa Stars yaichapa Afrika ya Kati".
  16. Allen, Neil (2022-09-20). "Pompey youngster's sacrifice to demonstrate commitment to struggling Gillingham". www.portsmouth.co.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-23.
  17. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named sw