Nenda kwa yaliyomo

Elizabeth Ann Seton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elizabeth Ann Seton.

Elizabeth Ann Bayley Seton (28 Agosti 17744 Januari 1821) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista wa Huruma wa Mt. Yosefu (kwa Kiingereza: Sisters of Charity of St. Joseph), ambalo lilikuwa utawa wa kwanza kuundwa huko Marekani. Hasa alifundisha na kuwasaidia watoto maskini wengi.

Mchakato wa kumtangaza mwenyeheri ulianza mwaka 1907 na kumalizika Papa Yohane XXIII alipomtangaza mwenye heri tarehe 17 Machi 1963.

Tarehe 14 Septemba 1975 Papa Paulo VI alimtangaza kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni 4 Januari[1].

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Elizabeth Ann Bayley alizaliwa New York katika familia ya ushirika wa Anglikana.

Tarehe 25 Januari 1794, akiwa na umri wa miaka 19, aliolewa na mfanyabiashara tajiri William Seton, akamzalia watoto watano.

Alipobaki mjane tarehe 27 Desemba 1802) alifunga safari ya kiroho iliyomfanya aongokee Kanisa Katoliki tarehe 25 Machi 1805.

Akahamia Baltimore, chini ya askofu John Carroll, akaanza utume wake kwa wanawake wajane wenye watoto wadogo na kuanzisha shule nyingi kwa ajili ya malezi ya mabinti na wavulana fukara[2].

Tarehe 1 Juni 1809 alianzisha shirika la kitawa lenye kufuata roho ya Vinsenti wa Paulo akahamia Emmitsburg, kwenye Maryland.

Mwaka 1812 alipokea katiba ya Mabinti wa Upendo wa Mt. Vinsenti wa Paulo, iliyorekebishwa na kuidhinishwa na askofu Carrol.

Kundi la kwanza la masista (mama Seton na wenzake 16) waliweka nadhiri za daima tarehe 19 Julai 1813.

Alifariki mwaka 1821.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]