Dayron Robles
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Robles akiongoza katika fainali ya mbio ya 110m ya urukaji viunzi katika Olimpiki ya Beijing ya 2008 | ||
Riadha ya Wanaume | ||
Anawakilisha nchi Cuba | ||
Michezo ya Olimpiki | ||
Dhahabu | 2008 Beijing | 110 m ya urukaji viunzi |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi | ||
Fedha | 2006 Moscow | 60 m urukaji viunzi |
Dayron Robles (alizaliwa Guantanamo, Cuba, 19 Novemba 1986) ni mwanariadha wa kuruka viunzi ambaye anashikilia rekodi ya mbio ya 110m ya kuruka viunzi kwa muda wa sekunde 12.87.Aliweka rekodi hii mnamo 12 Juni 2008 katika mashindano ya Golden Spike Ostrava na yeye ndiye Bingwa wa Olimpiki wa sasa.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani jijini Moscow,alichukua nafasi ya pili kwa muda bora wa kibnafsi(mbio za ndani) wa 7.46s,muda huu ameuboresha sasa ukawa 7.33s(huu ndio muda wa kasi wa pili duniani katika mbio hii ,akiwa nyuma ya Colin Jackson).
Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2008 mjini Valencia,hakuhitimu kuingia fainali kwa sababu alisimama alipodhani kuwa mwanariadha mwenzake,Liu Xiang alikuwa ameanza mbele ya wengine. Hii ilikuwa bahati mbaya sana kwa Robles,aliyekuwa amekimbia muda tisa kati za muda 11 kasi kabisa katika msimu huo na alikuwa akionekana ni kama atashinda medali ya dhahabu.
Katika michezo ya Olimpiki ya Beijing katika mwaka wa 2008, watu walitarajia mashindano makali kati ya Robles na Liu katika fainali.Liu alishindwa kuendelea baada ya kupata jeraha katika mbio ya kuhitimu kutokana na tendinitis. Robles alishinda fainali kwa urahisi sana kwa muda wa 12.93s na kushinda medali ya dhahabu.
Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009,Robles alitoka na hakumaliza mbio za nusu fainali kwa sababu ya jeraha la misuli.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Muda bora wa binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mashindano | Muda (sekunde) | Pahali pa kushindana | Tarehe |
---|---|---|---|
50 m urukaji viunzi | 6.39 | Stockholm, Uswidi | 21 Februari 2008 |
60 m urukaji viunzi | 7.33 | Düsseldorf, Ujerumani | 8 Februari 2008 |
110 m urukaji viunzi | 12.87 rekodi ya dunia katika mbio hii hadi sasa | Ostrava, Czech | 12 Juni 2008 |
- Habari yote kutoka IAAF[1] Archived 5 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
Katika Mashindano
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Shindano | Pahali pa Kushindana | Matokeo | Mbio ya |
---|---|---|---|---|
2003 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Vijana | Sherbrooke, Kanada | 6 | 110 m urukaji viunzi |
2004 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Vijana ya 2004 | Grosseto, Uitalia | 2 | 110 m urukaji viunzi |
2005 | Mashindano ya Mabingwa wa Amerika ya Kati na Visiwa vya Carribean | Nassau, Bahamas | 2 | 110 m urukaji viunzi |
2006 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi ya 2006 | Moscow, Urusi | 2 | 60 m urukaji viunzi, 7.46 s |
Michezo ya Amerika ya Kati na Visiwa vya Carribean ya 2006 | Cartagena, Colombia | 1 | 110 m urukaji viunzi, 13.12 s | |
2007 | Michezo ya PanAmerika | Rio de Janeiro, Brazili | 1 | 110 m urukaji viunzi, 13.25 s |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia Katika Riadha ya 2007 | Osaka, Ujapani | 4 | 110 m urukaji viunzi, 13.15 s | |
Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Fainali ya IAAF ya 2007 | Stuttgart, Ujerumani | 1 | 110 m urukaji viunzi, 12.92 s | |
2008 | Mashindano ya Golden Spike | Ostrava, Czech | 1 | 110 m urukaji viunzi, 12.87 s |
Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 1 | 110 m urukaji viunzi, 12.93 s |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "World Indoor Championship Results".
- "Liu Xiang to meet Robles in World Champs".
- Frederik Balfour (August 18, 2008). "China Olympic Hero Liu Xiang Quits Games". BusinessWeek.
- "Merritt of U.S., Cuba's Robles capture track gold".
- "Robles, Dayron biography". IAAF. Archived 5 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Dayron Robles
- IAAF "Focus on Athletes" article Archived 26 Oktoba 2011 at the Wayback Machine.
Alitanguliwa na Liu Xiang |
Wanaume walioshikilia rekodi ya 110m ya urukaji viunzi 12 Juni 2008 – |
Akafuatiwa na Yeye ndiye Bingwa Mtetezi |
Alitanguliwa na Liu Xiang |
Mwanaume Bora wa mbio ya 110m ya Urukaji viunzi wa mwaka 2007 (akiwa pamoja na Liu Xiang), 2008 |
Akafuatiwa na Yeye ndiye Bingwa Mtetezi |
Alitanguliwa na Asafa Powell |
IAAF Mtendaji bora wa mwaka 2008 |
Akafuatiwa na Yeye ndiye Bingwa Mtetezi |