Nenda kwa yaliyomo

Chillingham Castle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngome ilivyochorwa katika karne ya 19.

Ngome ya Chillingham ni ngome ya kipindi cha Enzi ya Kati katika historia iliyoko kwenye kijiji cha Chillingham kwenye kaskazini ya Northumberland, Uingereza. Katika ngome hii wanapatikana ng'ombe wa aina adimu sana ya Ng'ombe wa Chillingham.[1] The castle is a Grade I listed building.[2]

Yalikuwa ndio makazi ya Grey na Bennett toka karne ya 15 hadi miaka ya 1980 ilipokuwa makazi ya Sir Edward Humphry Tyrrell Wakefield.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ngome hii awali ilikuwa ni monasteria mwishoni mwa karne ya 12. Mwaka 1298, Mfalme Edward I alikaa kwenye ngome hii wakati akielekea Uskochi kupigana na jeshi la Uskochi lililoongozwa na William Wallace.

Ngome hii ilitumiwa kama mahali wanajeshi wa Uingereza walipoanzisha vita dhidi ya Uskochi.

Anne wa Denmark na watoto wake walikaa kwenye ngome hii wakati wa safari yao ya kwenda London Juni 6, 1603.[3] Mwaka 1617, Mfalme James I wa Uingereza, ambaye utawala wake uliunganisha Uingereza na Uskochi alikaa hapo wakati akisafiri kati ya nchi hizi mbii.

Wakati wa vita za Kwanza na Pili za Dunia, ngome hii ilitumika kama kituo cha jeshi. Inaaminika kuwa kipindi hiki ndio wakati ambao mbao zilizotumika kupendesha ngoma ziliondolewa na kuchomwa moto na wanajeshi. Baada ya vita, ngome ilianza kuharibika. Sehemu kubwa iliharibika kutokana na kuvuja kwa paa. Mwaka 1982, ngome ilinunuliwa na Sir Humphry Wakefield, ambaye mke wake Catherine alitoka katika familia ya Grey wa Chillingham waliokuwa wamiliki wa kwanza.

Mizimu ya Chillingham

[hariri | hariri chanzo]
Lady Mary Berkeley, ambaye sauti yake huaminika kusikika ndani ya ngome

Wamiliki wa sasa wa ngome hii wanaitangaza kuwa ni ngome yenye kutembelewa na mizimu kuliko ngome yoyote Uingereza.[4][5] Imefanyiwa uchunguzi na kuwa kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni, radio na YouTube,[6] I'm Famous and Frightened!, Scariest Places On Earth, Holiday Showdown, Alan Robson's Nightowls), The ParaPod, ‘'Ghost Hunters International, A Blood Red Sky (2013).

Mzimu maarufu katika ngome hii ni "blue boy".[7] Watu wanaotembelea ngome hii hudai kuona miale ya bluu juu ya vitnda vyao.

Kwenye Fasihi

[hariri | hariri chanzo]

Ngome hii iko katika vitabu mbalimbali kama vile The Bride of Lammermoor (1819) kilichoandikwa na Sir Walter Scott. Ngome hii ndio iliyopelekea kuandikwa kwa kitabu cha watoto na Eva Ibbotson's mwaka 2005 cha The Beasts of Clawstone Castle.[8][9]

  1. "Coming up on this week's Countryfile - Sunday 1 November". Countryfile. BBC. 30 Oktoba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-09. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Chillingham Castle". Heritage Gateway (English Heritage, Institute of Historic Building Conservation and ALGAO:England). 2006. Iliwekwa mnamo 6 Agosti 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. HMC Salisbury Hatfield, vol. 15 (London, 1930), p. 126.
  4. "Ghosts". Chillingham Castle. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-09. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Wakefield, Mary (29 Oktoba 2004). "The ghosts of a chance". The Daily Telegraph. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Smith, Ian. "Castle's ghostly reputation leads to expansion plans", 12 April 2007. Retrieved on 9 October 2017. Archived from the original on 2017-10-09. 
  7. Campbell Dixon, Anne (24 Juni 2000). "Northumberland: Castle's knight in shining armour". The Daily Telegraph. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Whetstone, David. "Eva just gets better", 17 May 2005. Retrieved on 2019-07-16. Archived from the original on 2015-02-15. 
  9. "Obituary: Eva Ibbotson", 25 October 2010. Retrieved on 2019-07-16. Archived from the original on 2019-07-16. 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Uingereza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chillingham Castle kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.