Nenda kwa yaliyomo

Berhaneyesus Demerew Souraphiel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Berhaneyesus Demerew Souraphiel, C.M. (alizaliwa 14 Julai 1948) ni kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki la Waethiopia, ambalo amekuwa akiliongoza tangu alipochaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Addis Ababa mwaka 1999. Pia ni chansela wa Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika ya Mashariki na rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Ethiopia na Eritrea. Mnamo mwaka 2015, aliteuliwa kuwa kardinali na Papa Fransisko.

Akiwa kuhani, alifungwa gerezani na serikali ya Kikomunisti ya Ethiopia kati ya mwaka 1979–1980. Kama mwanachama wa Shirika la Wamisionari wa Mtakatifu Vinsenti wa Paulo (Congregation of the Mission), aliwahi kusimamia nyumba ya malezi ya shirika hilo katika miaka ya katikati ya 1980 na kuwa mkuu wa kanda ya shirika (provincial superior) kuanzia mwaka 1990 hadi 1994.

Alihudumu kama askofu msaidizi wa Addis Ababa kwa miezi 18 kabla ya kuteuliwa kuwa askofu mkuu.[1]

  1. "Nomina dell'Arcivescovo Metropolita di Addis Abeba (Etiopia)". Daily Bulletin (kwa Kiitaliano). Rome: Holy See Press Office. 7 Julai 1999. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Aprili 2013. Iliwekwa mnamo 1 Februari 2013.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.