Bendera ya Ghana
Bendera ya Ghana ina milia mitatu ya kulala ya rangi nyekundu, dhahabu na kijani pamoja na nyota nyeusi katikati. Hizi ni rangi za Ethiopia zinazoitwa pia rangi za Umoja wa Afrika. Bendera ya Ethiopia ilikuwa ya kwanza katika Afrika ya kurudia rangi hizi na nchi nyingi zilifuata.
Imetumika tangu 1957. Kati ya 1964 hadi 1966 ilibadilishwa kwa kufanya mlia wa katikati mweupe. Bendera imetungwa na Mrs. Theodosia Salome Okoh kwa ajili ya sherehe ya uhuru mwaka 1957.
Mara nyingi rangi zinaelezwa kwa njia hiyo: nyekundu kama rangi ya damu iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi, dhahabu kwa ajili ya utajiri wa madini na kijani kwa ajili ya misitu na kilimo.
Nyota nyeusi inasemekana imetoka katika nembo ya kampuni ya usafiri kwa meli ya Black Star Line iliyokuwa chini ya Marcus Garvey kuanzia 1919 hadi 1922.