Aust-Agder
Aust-Agder ni moja kati ya Majimbo ya Norwei (fylke). Imepakana na Telemark, Rogaland, na Vest-Agder. Kunako mwaka wa 2002, kulikuwa na wakazi takriban 102,945, ambayo ni 2.2% ya jumla ya idadi ya wakazi wa nchini Norwei. Ni kweli ina kilomita za mraba zupatazo 9,212 (3,557 sq mi). Kitovu cha utawala wa jimboni hapa ni mjini Arendal.
Jimbo, ambalo lipo katika pwani ya Skagerrak, linatoka Gjernestangen hadi Risør hadi Kvåsefjorden hadi Lillesand. Sehemu za ndani za maeneo yake ni pamoja na Setesdalsheiene na Austheiene. Takriban 77% ya wakazi wake wanaishi katika eneo la pwani, ambapo ndipo kuna ujenzi mkubwa kabisa. Utalii ni muhimu mjini hapa, kama jinsi ilivyo Arendal na miji mingine ya pwani ni vivutio maarufu.
Jimbo hili linajumuisha kisiwa cha Tromøy, Justøya, na Sandøya. Ndani ya jimbo linajumuisha wilaya ya Setesdal, kupitia mto Otra unaomwagikia baharini.
Manispaa zake
[hariri | hariri chanzo]Aust-Agder imegawanyika katika manispa 15:
Ukubwa | Jina | Wakazi | Eneo km² | Map |
---|---|---|---|---|
1 | Arendal | 41,655 | 256 | |
2 | Grimstad | 20,497 | 273 | |
3 | Lillesand | 9,465 | 180 | |
4 | Risør | 6,894 | 179 | |
5 | Tvedestrand | 5,939 | 204 | |
6 | Froland | 5,002 | 605 | |
7 | Birkenes | 4,689 | 633 | |
8 | Evje og Hornnes | 3,397 | 521 | |
9 | Gjerstad | 2,478 | 308 | |
10 | Vegårshei | 1,886 | 322 | |
11 | Åmli | 1,861 | 1,068 | |
12 | Valle | 1,289 | 1,135 | |
13 | Iveland | 1,254 | 250 | |
14 | Bygland | 1,223 | 1,156 | |
15 | Bykle | 970 | 1,256 | |
Jumla | Aust-Agder | 108,499 | 9,158 |
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Political map Archived 6 Aprili 2016 at the Wayback Machine.
- Aust-Agder fylkeskommune (in English) Archived 9 Machi 2004 at the Wayback Machine.
- Photogallery Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
58°34′00″N 08°34′00″E / 58.56667°N 8.56667°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aust-Agder kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |