Atalia
Mandhari
Atalia (kwa Kiebrania: עֲתַלְיָה, ʻĂṯalyâ, "Mungu anainuliwa"[1]) alikuwa malkia wa ufalme wa Yuda kama mke wa mfalme Yehoramu wa Yuda, aliyekuwa wa ukoo wa David.
Baada ya huyo kufa, alijitwalia madaraka kinyume cha taratibu na kwa ukatili mkubwa (2Fal 11:1)[2] akatawala miaka 841–835 KK, mpaka alipopinduliwa na kuuawa (2Fal 11:14-16; 2Nya 23:12-15).
Binti au dada wa mfalme Ahabu wa Israeli, alijitahidi kueneza ibada kwa Baali na miungu mingine dhidi ya YHWH, Mungu pekee wa dini ya Musa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ H. J. Katzenstein, "Who Were the Parents of Athaliah?" Israel Exploration Journal 5 (1955) 194-197; Winfried Thiel, "Athaliah" in Anchor Bible Dictionary, David Noel Freedman and Gary A. Herion, editors (New York: Doubleday, 1992) 511-512; and R.C. Klein "Queen Athaliah daughter of Ahab or Omri", Jewish Bible Quarterly 42:1 (2014) (available online on Reb Chaim HaQoton
- ↑ Brenner, Athalya. "Athaliah", Jewish Women's Archive
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Atalia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |