AK-47
Bunduki ya Kalashnikov (Калашников) au AK-47 ni aina ya bunduki inayofuata muundo uliobuniwa na mvumbuzi Mikhail Kalashnikov kutoka nchini Urusi. Kuna matoleo tofauti ya bunduki hizo.
Hapo awali zilitengenezwa katika Umoja wa Kisovyeti, lakini bunduki hizo na anuwai zao sasa zinatengenezwa katika nchi nyingi.
Kalashnikov ni mojawapo ya bunduki zinazotumiwa sana ulimwenguni kote; kwa jumla kuna bunduki milioni 72 zinazopatikana katika nchi karibu 100. [1] [2]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uongozi wa Jeshi Jekundu (jeshi la Umoja wa Kisovyeti) ulitambua wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia dhidi ya Ujerumani kwamba inahitajika bunduki mpya inayoweza kutumiwa kwa kufyatua risasi moja-moja lakini pia kwa wingi ikifaa, kwa namna ya bombomu.
Katika mashindano yaliyotangazwa ndani ya jeshi na tasnia ya silaha, Mikhail Kalashnikov alishinda. Modeli yake ilikuwa tayari mwaka 1947 ikaanza kutengenezwa mwaka 1948. Kifupi AK-47 kinamaanisha "Avtomat Kalashnikov 1947" (Автомат Калашникова складной образца 1947 года).
Ni bunduki ambayo inatengenezwa kwa urahisi, inafanya kazi pia katika mazingira magumu kama joto au baridi kali, mvua au ukame. Hivyo imesambaa sana duniani, na uongozi wa Umoja wa Kisovyeti ulitoa vibali kwa nchi nyingi rafiki ya kuinakili na kuitengeneza kwao.
Uzalishaji
[hariri | hariri chanzo]Ubunifu rahisi wa bunduki hufanya iwe rahisi kutolewa, na Umoja wa Kisovyeti ulikodisha mipango ya silaha hiyo kwa nchi rafiki, ambapo ingeweza kutengenezwa kienyeji kwa gharama ya chini. [3] Kama matokeo, bunduki za Kalashnikov na anuwai zao zimetengenezwa katika nchi nyingi, na bila leseni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Franko, Blake (2017-05-08). "The Gun That Is in Almost 100 Countries: Why the AK-47 Dominates". The National Interest (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-26.
- ↑ McCarthy, Niall. "The Cost Of An AK-47 On The Black Market Around The World [Infographic]". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-26.
- ↑ Franko, Blake (2017-05-08). "The Gun That Is in Almost 100 Countries: Why the AK-47 Dominates". The National Interest (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-26.Franko, Blake (2017-05-08). "The Gun That Is in Almost 100 Countries: Why the AK-47 Dominates". The National Interest. Retrieved 2019-09-26.
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Michael Hodges (2007). AK47: The Story of a Gun. MacAdam/Cage Pub. ISBN 978-1-59692-286-0.
- Joe Poyer (2006). The AK-47 and AK-74 Kalashnikov Rifles and Their Variations: A Shooter's and Collector's Guide. North Cape Publications. ISBN 978-1-882391-41-7.
- Gordon L. Rottman (2011). The AK-47: Kalashnikov-series assault rifles. Bloomsbury Publishing. ISBN 978-1-84908-835-0.
- Martin J Brayley (2013). Kalashnikov AK47 Series: The 7.62 x 39mm Assault Rifle in Detail. Crowood. ISBN 978-1-84797-526-3.
- Duncan Long (1 Septemba 1988). AK47: The Complete Kalashnikov Family Of Assault Rifles. Paladin Press. ISBN 978-0-87364-477-8.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |