,

Malengo Quotes

Quotes tagged as "malengo" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu – Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi (ubinadamu), si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu au kama mtu binafsi, kujenga jengo la ofisi, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa kampuni au nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika kitu chochote kile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili wanaweza kutawaliwa. Ishirini na mbili hadi ishirini na nne wanaweza kukuumiza. Ishirini na nne hadi ishirini na saba unaweza kuweka malengo nao yenye natija. Ishirini na saba hadi thelathini watakuchunguza sana na hawatakupenda kutoka moyoni. Thelathini hadi thelathini na tano wamejawa na dharau za kijinga. Thelathini na tano hadi arobaini na mbili watakung’ang’ania kupoza hasira za huko walikotoka. Tofauti na wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili, na wanawake wenye umri wa miaka ishirini na nne hadi ishirini na saba, wengine wote ni kubahatisha.”
Enock Maregesi