Nenda kwa yaliyomo

Waraka wa kwanza wa Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Agano Jipya

Waraka wa kwanza wa Petro ni kati ya vitabu 27 vinavyounda Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Mtume Paulo alipokaribia kumaliza kazi yake, wengine kati ya mitume na wanafunzi wao walianza kuandika kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Mmojawao ni Mtume Petro, kwa msaada wa Sila, akiwa Roma karibu na kuuawa katika dhuluma ya Kaisari Nero dhidi ya Wakristo (mwaka 64 hivi).

Baada ya kufanya utume huko Antiokia, na kabla ya kupitia Korintho kwenda Roma, aliweza kwa urahisi kutembelea mikoa ya Uturuki Kaskazini wa leo.

Wakristo wa huko ndio walioandikiwa barua hii yenye mafundisho na ibada kuhusu ubatizo na Pasaka.

Pamoja na hayo walihimizwa wasiogope maneno ya watu wengine wasiopendezwa na uongofu wao: hali ngumu ni fursa ya kulingana zaidi na Yesu mpole na mteswa (1Pet 1:1-12; 2:19-25; 3:13-5:14).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Tafsiri ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]

Ufafanuzi

[hariri | hariri chanzo]
  • The International Standard Bible Encyclopedia Ilihifadhiwa 1 Februari 2013 kwenye Wayback Machine.: 1 Peter
  • Easton's Bible Dictionary 1897: First Epistle of Peter
  • Ernst R. Wendland, “Stand Fast in the True Grace of God! A Study of 1 Peter" Ilihifadhiwa 7 Julai 2010 kwenye Wayback Machine.
  •  "Epistles of Saint Peter" . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  • 1 Peter The authenticity and authorship by Peter of the First Epistle of Peter defended
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa kwanza wa Petro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.